Saturday, 12 September 2015







 








Image copyrightRays
Image captionMlipuko wa gesi waua 25 India
Polisi nchini India wanasema kuwa watu 20 waweuawa wakati mtungi wa gesi ulipolipuka katika hoteli moja iliyo jimbo la Madhya Pradesh.
Hoteli hiyo iliyokuwa karibu na kituo cha mabasi ilikuwa imejaa wafanyikazi na watoto wa shule waliokuwa wakipata kiamsha kinywa.
Waokoaji walitumia mikono yao wakiwatafuta manusura kwenye vifusi.
Majengo kadha yaliyokuwa karibu yaliharibiwa na mlipuko huo . Msemaji wa polisi anasema kuwa idadi ya waliokufa huenda ikaongezeka
Image copyrightAFP
Image captionKreni yaua 107 mjini Mecca
Gavana katika eneo la Mecca ameamrisha kufanyika uchunguzi kufuatia kuanguka kwa kreni katika msikiti mkubwa zaidi duniani.
Utawala nchini Saudi Arabia unasema kuwa upepo mkali ndio ulisababisha kreni iliyokuwa ikitumika kwa ujenzi kuanguka kwa msikiti mkubwa mjini mecca ambapo watu 107 waliuawa na wengine takriban 200 kujeruhiwa.
Image copyright
Image captionKreni yaua 107 mjini Mecca
Mkuu wa idara ya ulinzi wa angani nchini humo alisema kuwa kulikuwa na mvua kubwa wakati ajali hiyo ilipotokea na upepo ulikuwa ukivuma kwa takriban kilomita 83 kwa saa.
Msikiti huo unazunguka eneo takatifu la kiislamu la Kaaba na ndio msikiti mkubwa zaidi duniani na huwavutia mamia ya waislamu ambao huenda kuhiji kila mwaka.
Karibu watu milioni moja wamewasili nchini Saudi Arabia kabla ya sherehe za mwaka huu ambazo zinaanza wiki mbili zinazokuja.

Friday, 11 September 2015




Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akinadi sera zake kwa umati wa wakazi wa Mji wa Dodoma waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini humo leo Septemba 11, 2015, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Mikutano yake ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Benson Kigaila, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma leo Septemba 11, 2015.
10
Rais wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu Jaji Agustino Ramadhani akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa ndege wa Arusha ambapo alikutana na kuagana na majaji na watumishi wa Mahakama ya Afrika mjini Arusha leo.
11
9
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Rais wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu iliyopo mjini Aruha huku Rais wa Mahakama hiyo Jaji Agustino Ramadhani kulia akishuhudia.
2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Wa Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu Jaji Agustino Ramadhani wakizindua kitabu cha taarifa za msingi kuhusu mahakama hiyo kwenye Ukumbi wa Kibo kwenye majengo ya Mahakama hiyo mjini Arusha leo.Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuagana na viongozi na wafanyakazi wa mahakama hiyo.
5
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wafanyakazi na viongozi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu mjini Arusha leo.
78  
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Mahakama ya aFrika ya Haki za binadamu mjini Arusha wakati Rais alipotoa hotuba ya kuwaaga
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji na akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Isimani Iringa vijijini.Isimani Iringa vijijini,
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji na akihutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Isimani Iringa vijijini.Isimani Iringa vijijini,
Mgombea Mwenza wa Ukawa kupitia Chadema, Juma Duni Haji akiwa na mgombea ubunge jimbo la Isimani Iringa vijijini, Patrick Ole Sosopi

Thursday, 10 September 2015


Rais Jakaya Kikwete
TANZANIA imeendelea kusisitiza kuwa, Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, Wawakilishi, Madiwani na Masheha unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu utafanyika kwa amani na utulivu ambapo Watanzania watakuwa na uhuru wa kupiga kura bila woga kuwachagua viongozi wanaowataka.
Rais Jakaya Kikwete amesema furaha aliyonayo kumaliza salama kipindi chake cha uongozi na kujiandaa kukabidhi madaraka kwa rais ajaye, nchi bado ikiwa na umoja na mshikamano wa hali ya juu. Rais Kikwete ameyasema hayo  Ikulu, Dar es Salaam alipokutana na mabalozi wanne wapya wa nchi mbalimbali waliofika Ikulu kuwasilisha hati zao za utambulisho.
“Kampeni zinakwenda vizuri na tunategemea uchaguzi mkuu utakuwa wa amani na Watanzania watapata nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka,” Rais Kikwete amewaeleza mabalozi hao katika nyakati tofauti mara baada ya kupokea hati zao na kufanya nao mazungumzo.
Rais Kikwete ametumia nafasi hiyo kuwaeleza mabalozi kuhusu hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Mabalozi waliowasilisha hati zao jana tayari kuanza kuziwakilisha nchi zao Tanzania ni Florence Tinguely Mattli wa Uswisi, Yesmin Eralp wa Uturuki, Pekka Juhani Hukka wa Finland na Katarina Rangnitt wa Sweden.
Rais Kikwete pia amewahakikishia mabalozi hao kuwa Tanzania itaendeleza uhusiano mwema baina yake na nchi hizi ambazo ni rafiki na washirika wake wa maendeleo kwa miaka mingi.
danny-glover
Staa kutoka Marekani, Danny Glover katua Nigeria kwa kazi moja tu !! kama wewe ni mpenda movie kali kutoka Hollywood Marekani, jina la staa huyo sio geni…. kwenye list ya movie kali ziko na hizi hapa mtu wangu >>> ‘Legendary’ (2010- ndani yumo na John Cena pia), pamoja na movie ya ‘Rage’ ambayo amefanya na staa mwingine Nicolaus Cage (ilitoka mwaka 2014).
Taarifa ni kwamba mwigizaji  Danny Glover tayari katua Nigeria usiku wa September 08 2015 kwa ajili ya kuandaa  Movie ambayo itakuwa inahusu masuala ya Ebola, jina lake itaitwa ’93 DAYS’ ambayo ndani yake kutakuwa na story inayowahusu watu waliojitolea kupambana na Ebola.
tim-reid-close-up
Tim Reid
Kwenye list ya Mastaa watakaoigiza Movie hiyo yupo pia Tim Reid kutoka Hollywood Marekani pamoja na mastaa wengine kutoka Nigeria na Africa.
Image captionWatoto wa shule
Afrika Kusini imeanza kutekeleza sheria mpya, ambayo itaidhinisha majina ya wazazi ambao hawalipi malezi ya watoto kujumuishwa kwenye orodha ya watu wasiolipa madeni.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, watu hao wasiolipa hawatapewa mikopo na taasisi yoyote ya kifedha.
Lakini wakosoaji wa sheria hiyo wanasema kuwa itafanya hali ya maisha kuwa ngumu zaidi hasa kwa watu wa mapato ya chini.
Serikali ya nchi hiyo imesema sheria hiyo itawashurutisha wale ambao hawapi watoto wao msaada kufanya hivyo.
Baada ya shutuma nyingi, kipengee hicho kiliondolewa lakini kikarejeshwa tena na tayari rais Jacob Zuma ameisaini kuwa sheria.
Miongoni mwa wale wanaopinga sheria hiyo hiyo ni kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Party kinachoongozwa na Julius Malema, ambaye wafuasi wake wengi ni watu wenye mapato ya chini.
Idadi kubwa ya watu nchini Afrika Kusini, hasa watu masikini hutegemea mikopo kuendeleza maisha yao.

Wednesday, 9 September 2015





Image copyrightRays


Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza ametimiza miaka 63 katika enzi.
Huo ni muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza.Alitawazwa kuwa malkia akiwa na umri wa miaka 25 pekee.

Image captionAlipotawazwa

Mara ya kwanza alipofahamishwa kuwa ndiye atakayekuwa malkia wa Uingereza alikuwa nchini Kenya .

Image copyright
Image captionAkiwa na mumewe

Alikuwa katika ziara rasmi nchini Kenya akiwa na mmewe Philip wakati huo akiwa na umri wa miaka 25 pekee.

Image captionMalkia Elizabeth

Walikuwa wakikaa katika hoteli ya Treetops na jioni moja ikatangazwa kuwa babake amefariki akiwa usingizini.

Image copyrightRays
Image captionMalkia Elizabeth ofisini

Na hapo akawa Malkia lakini hakuambiwa habari hizo hadi alasiri siku iliyofuata.

Image copyrightRays
Image captionMalkia Elizabeth anawapenda mbwa

Mmewe alimpeleka katika ikulu ndogo ya Sagana na kumpa habari kwamba sasa ndiye malkia wa Uingereza.


Sasa miaka 63 baadaye Malkia anawashukuru sana wote waliomtumia ujumbe wa heri njema.

Image copyrightPA
Image captionMalkia Elizabeth akipokea salamu


Image copyrightRays
Image captionMalkia akiwa na mumewe Prince Phillip

Akizungumza karibu na mpaka wa Scotland Malkia Elizabeth 89 alisema ni heshima kubwa kwake kuendelea kuwahudumia waingereza.

Image captionMalkia Elizabeth ameweka rekodi ya kutawala kwa kipindi kirefu zaidi cha miaka 63

Malkia Elizabeth amehudumu kwa siku 23,226 , yaani miaka 63 .

Image copyrightRays
Image captionMalkia Elizabeth amehudumu kwa siku 23,226
Image copyrightrays
Image captionViongozi wengi wamesifu kwa unyenyekevu wake