Tuesday, 5 April 2016

                 EARY LIFE AND EDUCATION OF LOFVEN STEFAN

Lofven was born 21 July 1957 in Stockholm. He was placed in an organate 10 month after his birth. Lofven was later looked after by a foster family from Sunnersta  Sollwftea. Accordin to the agreement with this family his birth mother would regain custody of him when she was able to however this did not happen. After meeting his brother Stefan found out that his last name is Lofven (Spelled as Lofven in the Swedish population register)

Kjell Stefan Lofven, was born on 21 July 1957 in Stockholm Sweden, is a Swedish political who has been the Prime Minister of Sweden since the 3 Oct 2014 and before to get prime minister he studied at Solleftea Higher School before going on welding cause for 48 week at AMU in Kramfort Lofven studied social work at Umea University
BesigyeKiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye amezuiwa na maafisa wa polisi kuingia mji mkuu wa nchi hiyo Kampala.
Polisi wamemzuia alipokuwa katika makutano ya barabara za Mulago na Wandegeya karibu sana kuingia mji huo.
Wafuasi wake walikuwa wamekusanyika na polisi wametumwa kwa wingi eneo hilo.
Mwandishi wa BBC aliyeko Kampala Patience Atuhaire anasema polisi wamezuia watu kufuata gari la kiongozi huyo.
Gari ya Bw Besigye limebururwa na gari la polisi na kuelekezwa kituo cha polisi cha barabara ya Kira.
Maafisa wa polisi walikuwa wamesema Bw Besigye alikuwa na ruhusa kuingia mjini na kuhudhuria mkutano wa maombi katika makao makuu ya chama chake cha FDC kwa sharti kuwa asitatize shughuli mjini.
Bw Besigye amekuwa akizuiliwa nyumbani kwake Kisangati, viungani mwa mji wa Kampala, tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo Februari.
Mkuu wa polisi Kalekezi Kayihura aliagiza maafisa wa polisi waondokenyumbani kwa Bw Besigye Ijumaa iliyopita.
PICHA NA HABARI NI KWANIABA YA BBCSWAHILI.



















Monday, 4 April 2016

UturukiMaboti ya kwanza yaliyowabeba wahamiaji ambao wanafurushwa kutoka Ugiriki na kupelekwa Uturuki yameanza safari chini ya mpango wa EU unaotarajiwa kupunguza idadi ya wahamiaji wanaoingia Ulaya.
Mamia ya wahamiaji wameonekana wakiabiri feri katika kisiwa cha Lesbos nchini Ugiriki mapema Jumatatu.
Wanapelekwa Dikili, magharibi mwa Uturuki.
Maafisa wa Uturuki wamesema wanatarajia kupokea karibu watu 500.
Mkataba kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki umeshutumiwa vikali na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu na kuna wasiwasi pia kuhusu maandalizi duni.
Wahamiaji nchini Ugiriki wamelalamika kwamba hawana habari za kutosha kuhusu utaratibu wa kuomba hifadhi na wengine wamesema hawafahamu kwamba wanaweza kurejeshwa Uturuki.
Idara ya EU inayohusika na kuwasindikiza watu na kuwavusha bahari ya Aegean ina chini ya asilimia kumi ya wafanyakazi inaohitaji kutekeleza jukumu hilo, shirika la habari la Associated Press limeripoti.
Feri nyingine inayobeba wahamiaji kuwapeleka Uturuki inatarajiwa kuondoka kisiwa cha Chios nchini Ugiriki baadaye Jumatatu.MkatabaChini ya mkataba huo wa EU, wahamiaji wanaowasili kwa njia haramu Ugiriki wanatarajiwa kurejeshwa Uturuki wasipowasilisha maombi ya kutafuta hifadhi au maombi yao yakikataliwa.
Kwa kila mhamiaji wa Syria anayerejeshwa Uturuki, EU inapangiwa kumpokea mhamiaji mwengine wa Sryia ambaye ombi lake limekubaliwa.
Uturuki itanufaika kifedha na kisiasa kutoka kwa umoja huo chini ya mkataba huo.
Tangu kutiwa saini kwa mkataba huo mwezi Machi karibu watu 400 wamekuwa wakiwasili kila siku visiwa vya Ugiriki.
Wahamiaji milioni moja waliingia Ulaya kupitia Ugiriki kwa kutumia maboti kutoka Uturuki mwaka jana.
KWAHISANI YA BBC SWAHILI
Jeshi la Nigeria limesema kuwa limemkamata kiongozi wa kundi wapiganaji wa Kiislam la Ansaru lenye uhusiano pia na kundi la kigaigi la Al Qaeda.taarifa ya msemaji wa jeshi la Nigeria Brigedi Jenerali Rabe Abubakar inasema kuwa Khalid al-Barnawi alikamatwa katika jimbo la Kogi nchini Humo.
Kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kundi la Ansaru tawi la Boko Haram kunafuatiwa kusakwa kwa muda mrefu ambapo Marekani walitoa ahadi ya zawadi ya dola millioni tano kwa yeyote atakayefanikisha kutiwa nguvuni Khalid al Barnawi.
Ansaru ni kundi maarufu kwa utekaji wa raia kutoka nchi za Magharibi na limekuwa likituhumiwa kwa mauaji ya raia kadhaa wa kimagharibi pia.Brigedia Jenerali Rabe Abubakar ameiambia BBC kuwa kukamatwa kwa Barnawi ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi.
“Ndiyo tumemkamata gaidi.Yeah, kukamatwa kwake ni hatua kubwa katika vita dhidi ya ugaidi,na si ndani ya Nigeria tu bali duniani kote pia. Ni mtu mhimu sana katika makundi ya kigaidi Nigeria na Duniani,na tunajitahidi kuhakikisha hatuishii kumkamata yeye tu bali na wengine.
Kwa Hisani Ya BBC SWAHILI
MvuaWatu 60 wamefariki kutokana na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha maeneo ya kaskazini magharibi mwa Pakistan, maafisa wanasema.
Mvua kubwa ilianza kunyesha Jumamosi na kusababisha mafuruiko mikoa ya Khyber Pakhtunkhwa, Kashmir na Gilgit Baltistan.
Ingawa msimu wa mvua za pepo za msimu haujaanza, mvua za kabla ya msimu mara nyingi husababisha uharibifu hasa maeneo ya mashambani Pakistan ambapo miundo mbinu ni duni.MvuaMaafisa wamesema wakazi wametakiwa waondoke na kukimbilia nyanda za juu na maeneo yaliyo salama.
Mwaka uliopita, zaidi ya watu 170 waliuawa wakati wa msimu wa mvua za masika nchini Pakistan.
Google imelazimika kuondoa kitufe cha Siku ya Wajinga kutoka kwenye huduma yake ya barua pepe ya Gmail baada ya watu wengi kulalamika.
Kitufe hicho kilikuwa kinatuma video za mzaha kwa watu walio kwenye anwani ya mtu.
Kitufe hicho kilikuwa kimewekwa karibu na kitufe cha kawaida cha kutuma barua pepe na kiliwawezesha watumizi wa Gmail kusitisha mawasiliano ya kawaida na badala yake kutuma video fupi ya gif ya kibonzo kikiweka chini maikrofoni.
Watu wengi wamelalamika sana kuhusu kitufe hicho kwenye kumbi za Google.
Kuna wanaosema wamefutwa kazi baada ya kuwatumia wakubwa wao barua pepe za mzaha, wengine wanasema wametuma barua pepe za mzaha kwa kampuni ambazo walikuwa wanaomba kazi.
Mwandishi mmoja aliandika kwamba alikuwa anataka kutuma makala zake kwa mhariri na muda ulikuwa unapita akatuma haraka. Alisubiri jibu lakini hakupata. Baadaye aligundua kwamba kimakosa alibofya kitufe cha mzaha.
Kampuni hiyo imeondoa kitufe hicho na kuomba radhi.
"Inaonekana kana kwamba tumejitania sisi wenyewe mwaka huu,” Google imesema kupitia taarifa.
"Kutokana na hitilafu katika utengenezaji wa kitufe hiki, kiungo cha kuweka maikrofoni chini (MicDrop) kilisababisha kilio kuliko kicheko. Tunaomba radhi.”
Google ilitangaza kuanzishwa kwa Gmail tarehe 1 Aprili 2004 na wakati huo wengi walidhani ulikuwa mzaha wa Siku ya Wajinga.Google