Friday, 6 May 2016

Picha za gari lililokuwa na ujumbe wa kukasirisha uliochorowa katika gari hilo zimesambazwa mara elfu katika mtandao wa Twitter.
Gari hilo jeupe aina ya Range Rover Revere lenye bei ya pauni 75,000 lilionekana limeegeshwa karibu na Harrods magharibi mwa London na kuchorwa ujumbe wa kukasirisha kwa kile kilichoonekana kuwa mpenzi aliyedanganywa.
Gari hilo liliandikwa 'cheater' { mwongo} katika pande zote mbili za gari huku maneno ''Natamani angekuwa na thamani'' yakiandikwa katika madirisha ya gari hilo.
Klo ambaye alipiga picha za gari hilo alisema kuwa alimuona mwanamke mmoja akilichora gari hilo,alikuwa kama aliye na wazimu.
'Hakuna mtu aliyejaribu kumzuia.Baadaye aliondoka.Maneno ''Its Over'' pia yaliandikwa kwenye gari hilo ikielezea kuisha kwa uhusiano wowote''.
BurundiUhaba mkubwa wa mafuta umeshuhudiwa katika mji mkuu wa Bujumbura na maeneo mengine nchini Burundi.
Kwa karibu wiki moja sasa, vituo vya kuuza mafuta vimekabiliwa na uhaba mkubwa na wateja wanalazimika kupanga foleni kwenye vituo ambavyo bado havijamaliza mafuta.
Waziri wa nishati nchini humo aliambia runginga ya taifa Alhamisi kwamba hakuna sababu yoyote ya kuvifanya vituo vya mafuta kukosa mafuta ya kuuaza.
Alisema taifa hilo bado lina mafuta ya kutosheleza mahitaji.
Mwandishi wa BBC aliyeko Bujumbura Prime Ndikumagenge anasema licha ya hakikisho la waziri, uhaba bado umeendelea kushuhudiwa.
Baadhi ya watu wanasema huenda wanunuzi wa mafuta kwa wingi wameshindwa kupata fedha za kigeni za kutosha kuagiza petroli kutoka nje.
HABARI KWANIABA YA BBC SWAHILI.

Tuesday, 3 May 2016

JengoMtoto wa umri wa mwaka mmoja unusu amepatikana akiwa hai kwenye vifusi vya jengo lililoporomoka Ijumaa jijini Nairobi.
Jengo hilo la ghorofa sita liliporomoka katika mtaa wa Huruma baada ya mvua kubwa kunyesha.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, msichana huyo alitolewa kwenye vifusi mwendo wa saa kumi usiku na kukimbizwa hospitalini.
Kamanda wa kitengo cha taifa cha kudhibiti majanga Pius Maasai anasema hali ya mtoto huyo ni thabiti, kwa mujibu wa gazeti hilo.
Watu 22 wamethibitishwa kufariki na wengine karibu 90 hawajulikani walipo.
Juhudi za uokoaji bado zinaendelea siku ya nne baada ya mkasa huo kutokea.
Kufikia sasa, watu 136 wameokolewa.
Polisi wanasema wamiliki wa jumba hilo, ambalo maafisa wa baraza la jiji wanasema halikufaa kuishi watu, wamekamatwa na wanazuiliwa na polisi.
Taarifa zinasema watafikishwa mahakamani baadaye Jumanne.
HABARI KWANIABA YA BBCSWAHILI