Saturday, 16 January 2016

Eneo lililoshambuliwa.

Rais wa Burkina Faso amesema takriban watu 21 wameuwawa katika shambulio kwenye hoteli moja mjini Ogadugu na wanamgambo waliovamia hotel hiyo.
Roch Mark Christian Kabore amesema washambuliaji wanne waliovamia hotel hiyo waliuliwa ambapo wawili kati yao ni wanawake. Shambulio hilo lililotokea kwenye hotel ya Splendide kwenye mji mkuu wa Ouagadougou sasa limemalizwa.Baadhi wa Manusura.
Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo amesema wanamgambo hao wameuwa watu kumi na nane kutoka mataifa mbalimbali. Zaidi ya watu mia moja na ishirini walikimbia hotel hiyo maarufu kwa watalii.
walionusurika wanasema wanamgambo hao walianza kupiga risasi kwenye jengo hilo na kisha kuliwasha moto.Wanajeshi Maalumu wa Ufaransa.
Kundi la Kigaidi la Al Qaeda kwenye ukingo eneo jangwa imesema lina husika na shambulio hilo.
Watu 126 waliokuwa mateka waliachiliwa huru katika hoteli ya Splendid iliopo katika mji mkuu wa taifa hilo la Magharibi mwa Afrika Ouagadougou, kwa mujibu wa waziri wa maswala ya ndani.Eneo la Jirani ya Hoteli ya Spendid
Wapiganaji wanne waliuawa aliongezea huku watu 21 wa mataifa 18 tofauti wakifariki wakati wa shambulio ambalo pia liliulenga mgahawa huo.
Vikosi maalum vya Ufaransa vinasaidia wanajeshi wa taifa hilo katika oparesheni hiyo.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameshtumu shambulio hilo la taifa hilo ambalo lilikuwa koloni yake hapo zamani.
Kundi la Al-Qaeda la islamic Maghreb{AQIM} limesema kuwa lilitekeleza shambulio hilo katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika.Hoteli ya Splendid.
Mnamo mwezi Novemba shambulio la AQIM katika hoteli moja ya Bamako nchini Mali liliwauwa watu 19.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Kim Moon.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Bwana Ban ki Moon.

UMOJA wa Mataifa umeihadharisha Tanzania kuwa itakumbwa na mafuriko yatakayosababishwa na mvua za El-Nino na kutaka kuanza kuchukua tahadhari mapema.
Taarifa ya Umoja huo ya uwezekano mkubwa wa mafuriko yatakayosababishwa na mvua za El- Nino imetolewa wakati serikali inaendelea kubomoa nyumba zilizojengwa maeneo hatarishi katika mabonde na maeneo yasiyoruhusiwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi anayehusika na Misaada ya Kibinadamu na Uratibu wa Misaada ya Dharura, Stephen O’Brien, Tanzania inaweza kukabiliwa na mafuriko ya El-Nino kati ya mwezi huu wa Januari na Machi, mwaka huu.
Pamoja na Tanzania, nchi nyingine ambazo zimetajwa kukumbwa na mafuriko hayo makubwa ni pamoja na Madagascar, Malawi na Msumbiji. Taarifa ya O’Brien kuhusu madhara ya El-Nino na namna gani Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kujiandaa au inajiandaa na kadhia hiyo iliwasilishwa mbele ya wajumbe wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na nakala yake kutumwa kwa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Pamoja na kutoa tahadhari hiyo, O’Brien amezisihi nchi ambazo zinatarajiwa kukumbwa na maafa ya El -Nino kujiandaa ipasavyo na kuyataja maandalizi hayo kuwa ni pamoja na utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa wananchi watarajiwa wa athari za mvua hizo.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi, upande wa Afrika ya Mashariki, nchi kadhaa hususan ukanda wa magharibi zimekumbwa na uhaba mkubwa wa mvua na hivyo kuathiri kiwango cha upatikanaji wa chakula.
Nchi hizo ni Ethiopia, Sudan, Djibouti na Eritrea ilihali baadhi ya nchi zikipata kiwango cha mvua kilichovuka mipaka. “ Kuanzia mwezi Januari hadi Machi, nchi za Tanzania, Msumbiji, Madagascar na Malawi zina uwezekano mkubwa wa ku kumbwa na mafuriko ya El- Nino,” alisema O’Brien.
Alisema nchi hizo zitahitaji pamoja na mambo mengine misaada ya kujiandaa na kushughulikia kile kinachotabiriwa kwani kina uwezekano mkubwa wa kutokea. Ukiacha nchi za Afrika ya Mashariki, nchi nyingine kwa upande wa Afrika ambazo zimekumbwa na hali tete ya uhaba wa mvua na hivyo kutishia usalama na upatikanaji wa chakula ni Angola, Botswana, Malawi, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Zambia na Zimbabwe.
O’Brien alisema nchi hizo zimekuwa na uhaba wa mvua kiasi kwamba zitakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na kusababisha watu zaidi ya milioni 28 katika mataifa hayo kukukosa chakula.
Akizungumzia kuhusu misaada ambayo imekwishakutolewa na nchi wahisani ili kukabilia na ukame na madhara yatokanayo na El-Nino , Katibu Mkuu Msaidizi Mwandamizi huyo alisema kuwa hadi wakati anatoa taarifa yake kiasi cha Dola za Marekani milioni 360 kilikuwa kimetolewa na wafadhili kwa lengo la kukabiliana na madhara yatakayotokana na ElNino ikiwa ni pamoja na usalama wa chakula.
Pamoja na michango hiyo, O’Brien alisema haitoshi kutokana na ukweli kwamba maafa yatakayotoka na madhila ya El-Nino yanahitaji misaada zaidi. Mbali ya nchi za kanda ya Afrika baadhi ya nchi nyingine ambazo zitakumbwa na zilishawahi kupata balaa la El-Nino ni pamoja na nchi ambao zimo katika Bara la Latini Amerika na nchi za eneo la Pasifiki ambazo nyingi ni visiwa.
Shirika la Kimataifa la Hali ya Hewa (WMO) linatarajiwa Mwezi Februari kutoa taarifa zaidi kuhusu mwelekeo za mvua hizo za El-Nino. Mvua kama hizo zilishawahi kunyesha nchini Tanzania mwaka 1998 na kusababisha maafa makubwa na watu kadhaa walipoteza maisha, huku maelfu wengine wakijeruhiwa na kupoteza makazi.
Mwaka jana mwezi Agosti Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa tahadhari kuwa Tanzania ni kati ya nchi za Barani Afrika zitakazokumbwa na mvua za El Nino kati ya mwezi Septemba na Desemba, mwaka jana.
Meli ikiwa na shehena katika Bandari ya  Dar es Salaaam.SERIKALI imeendelea kuisafisha Bandari kwa kuwaondoa watendaji wa ngazi za juu na kuwahamishia wizarani ili kuongeza ufanisi katika utendaji, sambamba na kuongeza ukusanyaji wa mapato.
Wakati hayo yakitokea Bandari, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) amesimamishwa kazi huku Mhasibu Mkuu na Meneja Manunuzi wa taasisi hiyo wakihamishwa kwa tuhuma za kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato katika taasisi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuhusu mabadiliko Bandarini, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (pichani) alisema serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha inasimamia mapato ya serikali na taasisi zinafanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Aliwataja watumishi walioondolewa Bandari kuwa ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Peter Gawile, Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Killian Challe na Kaimu Mkurugenzi wa Manunuzi, Mashaka Kishanda.
Alisema watendaji hao wamerudishwa wizarani na itafanyika tathmini ili waangaliwe watapangiwa nafasi gani kwa kuwa inawezekana katika Bandari uwezo wao na ufanisi wao ulikuwa mdogo ila inawezekana maeneo mengine wakafanya vizuri zaidi.
Aidha alisema imewateua watendaji wengine kushika nafasi hizo akiwemo Anthony Mbilinyi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambaye anakwenda Bandari kushika nafasi ya Gawile, Benito Kalinga ambaye alikuwa Ofisa Manunuzi Mkuu wa TCRA anayeenda Bandari kushika nafasi ya Kishanda na Abdulrahaman Bamba ambae alikuwa TEHAMA Uchukuzi anayeenda kushika nafasi ya Challe.
“Tatizo kubwa lililokuwa linaonekana pale Bandari ni mfumo wa IT hivyo tumeamua hao waondoke… Tunaamini tukiwapa ushirikiano watendaji hawa wanaoingia watafanya vizuri zaidi na kufanikisha azma ya serikali ya kuongeza ukusanyaji wa mapato,” alisema.
Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Charles Chacha na kutaka kuhamishwa mara moja kwa Mhasibu Mkuu Alhaji Said Mteule na Meneja manunuzi wa taasisi hiyo, Said Kaswela kwa kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato katika taasisi hiyo.
Serikali pia imeona ifanye uchunguzi kuhusu ununuzi wa mtambo wa kufuatilia vyombo angani unaojulikana kama Automatic Data Surveillance-Broadcast (ADS-B) na mtambo wa kukusanya taarifa za usafiri wa anga (AMHS), ambayo imegharimu kiasi cha Euro milioni 1.5.
Mbarawa alitoa agizo hilo jana akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango pamoja na watendaji wa TCAA katika ziara aliyoizungumzia kuwa ni ya kuangalia uendeshaji na ukusanyaji wa mapato unavyofanyika katika taasisi hiyo.
Waziri huyo alisema kuna mambo yamejitokeza hivyo serikali imeona lazima ifanye uchunguzi kwenye ununuzi wa baadhi ya mitambo na pia imebaini kuna upotevu mkubwa wa ukusanyaji wa mapato ambao umechangiwa na uongozi wa taasisi kwa kutojipanga vizuri.
“Wizara imeamua Chacha kuanzia leo (jana), hataendelea na nafasi hiyo tena badala yake atatafutwa mwingine. Mhasibu Mkuu wa taasisi hii atahamishwa na ofisa wa manunuzi wa taasisi hii. Iko haja ya kumpeleka sehemu nyingine ili tupate mtu safi na makini,” alisema Waziri huyo.
Mitambo hiyo ilitakiwa kuanza kufanya kazi tangu Novemba mwaka jana, lakini mpaka sasa haijaanza kufanya kazi. “Bora ubaki na watu wawili kwenye kazi kuliko 10 ambao sio waadilifu,” alisema Mbarawa.
Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mpango alisema kikubwa wanachopigania ni kuhakikisha serikali inakusanya mapato yote ya kodi na yasiyo ya kodi na kuongeza kuwa taasisi hiyo ina vyanzo ambavyo vingeweza kuingizia serikali fedha nyingi.
“Mkaguzi Mkuu alikuja na kufanya utafiti lakini taarifa aliyoitoa haikufanyiwa kazi. Pia katika kudodosa inajulikana TCAA ina akaunti saba ambazo zinatia shaka,”alisema Waziri Mpango na kuagiza akaunti hizo kutokuguswa mpaka uchunguzi utakapofanyika.
“Nimeagiza ili fedha za taasisi hii zibaki salama isitoke hata senti, pia ndani ya wiki mbili ufanyike ukaguzi kubaini upotevu wote wa fedha za umma uliofanyika,” alisema na kuitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA), ifanye uchunguzi wa mchakato mzima wa ununuzi wa mitambo hiyo miwili ya ADSB na AMHS, pamoja na kusisitiza kuwa watumishi waliosimamishwa watahamishwa mara moja.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani(NECTA),Charles Msonde.

IKIWA wanafunzi 324,068 ambao ni asilimia 89.12 wakipata ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kuendelea na kidato cha Tatu, ufaulu wa masomo ya hisabati, fizikia, kemia na biashara uko chini ya wastani.
Aidha, wanafunzi 39,567 ambao ni asilimia 10.9 wameshindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo yao wakati mwaka 2014 wanafunzi 375,434 sawa na asilimia 92.66 walipata alama za kuendelea na masomo ya Kidato cha Tatu.
Hayo yamebainishwa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA), Dk Charles Msonde alipokuwa akitan gaza matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha Pili.
Alisema kati ya wanafunzi 324,068 ambao wamepata alama za kuendelea na masomo, wanafunzi 155, 667 ambao ni asilimia 42.80 wamepata ufaulu mzuri wa kiwango cha juu (Distinction), Ufaulu wa daraja la pili (Merit) na ufaulu wa daraja la tatu (Credit) wakati zaidi ya nusu (wanafunzi 168,401) wakipata daraja la nne la ufaulu (Pass) .
Kuhusu ufaulu wa masomo, Msonde alisema ufaulu katika masomo ya msingi ya kiswahili, biashara na kemia umepanda kidogo ukilinganisha na mwaka 2014 wakati ufaulu wa masomo ya Uraia, Historia, Jiografia, Kiingereza, Fizikia, Hisabati na Utun zaji vitabu (Book-Keeping) umeshuka kidogo ukilinganisha na mwaka 2014.
”Somo lililofanyika vizuri zaidi ni Kiswahili ambapo asilimia 86.34 ya wanafunzi waliofanya mtihani huo wamefaulu na somo lenye ufaulu wa chini zaidi ni Hisabati ambalo linaufaulu wa asilimia 15.21,” alisema.
Msonde aliongeza kuwa juhudi za makusudi zinahitajika kuendelea kufanyika ili kuinua kiwango cha ufaulu wa masomo ambayo yako chini ya wastani na kuyataja kuwa ni hisabati, fizikia, kemia na biashara.
Akizungumzia shule zilizofanya vizuri alisema ni Mwanza Alliance, Alliance Girls na Alliance Rock Army (Mwanza), St Francis Girls (Mbeya), Bethel Sabs Girls Mafinga (Iringa), Shamsiye, Feza Girls, Feza Boys na Canossa (Dar es Salaam) na Don Bosco Seminary ya Iringa.
Alizitaja shule 10 za mwisho na kuwa mikoa ya Tanga na Mtwara ndio imeongoza kuwa na shule ambazo hazijafanya vizuri. Shule hizo za mwisho ni Michenjele (Mtwara), Furaha (Dar es Salaam), Mdando, Mlongwema na Kwai (Tanga), Lionja (Lindi), Mkoreha (Mtwara), Mlungui (Tanga), Makong’onda (Mtwara) na Kwaluguru (Tanga).
Msonde aliwataja wanafunzi waliofanya vyema kwa kuangaliwa wastani wa pointi (GPA) kuwa ni Lineth Christopher (St. Aloysius Girls), Jerry Panga( Marian Boys) na Rhobi Simba (Marian Girls) Colin Emmanuel (Feza Boys), Nickson Maro (Magnificat), Diana Mwakibinga (Morning Stars), Elisha Peter (Buswelu), Gaudencia Lwitakubi (Alliance Girls), Fuad Thabit (Feza Boys) na Geraldina Kyanyaka (Canossa) Wasichana 10 bora ni Lineth, Rhobi, Diana, Gaudencia, Geraldina, Renata Chokola (St.Aloysius Girls), Happyness Mwailunga (Canossa), Monica Tesha (St.Aloysius Girls), Judith Amos (Precious Blood) na Amina Khalfani (Feza Girls).
Wakati wavulana 10 bora ni Jerry, Colin, Nickson, Elisha, Fuad, Mwinangwa Chibunde (Mwanza Alliance), Baraka Muhammed (Eagles), Joshua Kafula (Libermann Boys), Emmanuel Magombi (Morning Stars) na Frank Charles (Marist Boys)
Oparesheni ya kuizunguka hoteli moja iliovamiwa na wapiganaji imeisha ,serikali imetangaza,lakini ripoti zinaarifu kwamba hoteli nyengine iliopo karibu imeshambuliwa.
Watu 126 waliokuwa mateka waliachiliwa huru katika hoteli ya Splendid iliopo katika mji mkuu wa taifa hilo la Magharibi mwa Afrika Ouagadougou, kwa mujibu wa waziri wa maswala ya ndani.
Wapiganaji wanne waliuawa aliongezea huku watu 23 wa mataifa 18 tofauti wakifariki wakati wa shambulio ambalo pia liliulenga mgahawa huo.
Vikosi maalum vya Ufaransa vinasaidia wanajeshi wa taifa hilo katika oparesheni hiyo.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameshtumu shambulio hilo la taifa hilo ambalo lilikuwa koloni yake hapo zamani.
Kundi la Al-Qaeda la islamic Maghreb{AQIM} limesema kuwa lilitekeleza shambulio hilo katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika.
Mnamo mwezi Novemba shambulio la AQIM katika hoteli moja ya Bamako nchini Mali liliwauwa watu 19.
Raisi Mteule wa Taiwani,Bi Tsai Yingwen.
Mgombea anayeunga mkono harakati za uhuru kwenye taifa la Taiwan Tsai Yingwen kutoka chama cha Democratic Progressive ameshinda uchaguzi wa urais nchini humo.
Chama tawala cha Kuomintang ambacho kinapendelea ushirikiano na upande wa bara wa taifa la Uchina kimepoteza uchaguzi huo.
Baada ya nusu ya kura zote kuhesabiwa mpaka sasa, chama cha DPP kimeonyesha kuongoza kwa kishindo ikiwa wana zaidi ya asilimia 60 ya kura zote zilizopigwa mpaka sasa.
Bi Tsai atakuwa rais wa kwanza mwanamke kwenye dunia ya wazungumzaji wa lugha ya Kichina. Anatarajiwa kutoa hotuba ya ushindi punde.
Mwanidishi wa BBC mjini Taipei anasema ushindi wake unaweza kuanzisha mzozo na Uchina ambayo inaitazama Taiwan kama jimbo lake muhimu.

Friday, 15 January 2016

























Thursday, 14 January 2016