![Mali](http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/11/20/151120115406_radisson_mali_forces_4_512x288_afp_nocredit.jpg)
Friday, 20 November 2015
Posted by Unknown on 21:43:00
with No comments so far
Rais John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na mkewe Mary Majaliwa baada ya kumwapisha Waziri Mkuu kwenye ikulu ndogo ya Chamwinomjini Dodoma Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa kassim Majaliwa akipongezwa na Mbunge wa Isimani, William Lukuvi baada ya kuapishwa kwenye ikulu ya Chamwino mjini Dodoma Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akipongezwa na Mbunge wa Buchosa, Dkt.Charles Tizeba baada ya Waziri Mkuu, Majaliwa kassim Majaliwa kuapishwa kwenye ikulu ya Chamwino Dodoma Novemba 20, 2015. (picha na Ofisi ya Maziri Mkuu)
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akipongezwa na Mbunge wa Buchosa, Dkt.Charles Tizeba baada ya Waziri Mkuu, Majaliwa kassim Majaliwa kuapishwa kwenye ikulu ya Chamwino Dodoma Novemba 20, 2015. (picha na Ofisi ya Maziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa kassim Majaliwa akipongezwa na Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kuapishwa kwenye ikulu ya Chamwino mjini Dodoma Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akipongezwa na Baadhi ya waalikwa waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwake kwenye ikulu ndogo ya Cahamwino jijini Dar es salaam Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akipongezwa na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Sheikh Mtopa baada ya kuapishwa kwenye ikulu ndogo ya Chamwino jijini Dar es salaam Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akipongezwa na Baadhi ya waalikwa waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwake kwenye ikulu ndogo ya Cahamwino jijini Dar es salaam Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akipongezwa na Baadhi ya waalikwa waliohudhuria sherehe za kuapishwa kwake kwenye ikulu ndogo ya Cahamwino jijini Dar es salaam Novemba 20, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Posted by Unknown on 21:39:00
with No comments so far
![Mali](http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/11/20/151120115406_radisson_mali_forces_4_512x288_afp_nocredit.jpg)
Maafisa wa serikali ya Mali wamesema sasa hakuna mateka wowote waliosalia katika hoteli ya Radisson Blu mjini Bamako iliyokuwa imeshambulia asubuhi na watu wenye silaha huku miili ya watu 18 ikidaiwa kupatikana ndani ya hoteli hiyo.
Waziri wa usalama wa Mali Salif Traore ameambia kikao cha wanahabari kwamba watu wenye silaha walioshambulia hoteli ya Radisson kwa sasa hawazuilii mateka wowote.
Afisi ya rais wa Mali imeandika kwenye Twitter ikishukuru maafisa wa usalama na mataifa yaliyosaidia kukabiliana na shambulio hoteli hiyo ya kifahari.
Watu watatu wamethibitishwa kufariki na wanajeshi wawili kujeruhiwa.
Ubelgiji imesema afisa mmoja wa serikali yake ni miongoni mwa waliouawa kwenye shambulio hilo.
Geoffrey Dieudonne alikuwa Mali kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa serikali.
Uvamizi huo wa wanamgambo hao ulitekelezwa mapema asubuhi kwenye hoteli hiyo ya kifahari ambayo hupendwa sana na raia wa mataifa ya nje.Baadhi ya ripoti zilisema watu walioshambulia hoteli hiyo huenda wakafika 10.
Ufaransa ambayo imekuwa na wanajeshi Mali tangu 2013 ilituma wanajeshi wake kusaidiana na wanajeshi wa Mali. Aidha, polisi maalum wapatao 50 walitumwa kutoka Paris.
Kundi la wapiganaji wa kijihadi la al-Murabitoun limedai kuhusika kwenye shambulio hilo kupitia ujumbe kwenye akaunti ya Twitter ya kundi hilo, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ingawa habari hizo hazijathibitishwa. Kundi la Al-Murabitoun linajumuisha makundi mawili ambayo yalijitenga kutoka kwa tawi moja la al-Qaeda eneo la Afrika Kaskazini.
![](http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/624/amz/worldservice/live/assets/images/2015/11/20/151120120649_mali_hotel_attack_map624_swahili.jpg)
Ubalozi wa Marekani mjini Bamako umeandika kwenye Twitter kwamba unafahamu kuhusu shambulio hilo na kuwashauri wafanyakazi wake pahala salama nao raia wawasiliane na familia.
![](http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/624/amz/worldservice/live/assets/images/2015/11/20/151120090114_bamakousembassy.jpg)
Thursday, 19 November 2015
Posted by Unknown on 21:06:00
with No comments so far
Posted by Unknown on 20:56:00
with No comments so far
![](http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/05/13/150513185234_estadio_santiago_bernabeu_real_1_512x288_getty.jpg)
Mchezo huu wa wapinzani hawa uliobatizwa jina la El Clasico utachezwa katika dimba la Santiago Bernabeu huku mashabiki wapatao 80,000 wakitazama mchezo huo katika uwanja huo.
Huku kukiwa na ahadi ya ulinzi wa kutosha kutoka kwa Polisi na wanausalama, hii inakuaja baada ya kutokea mashambulizi ya kigaidi nchini Ufaransa wiki hii.
Mvuto mkubwa wa mchezo huu ni kuwepo kwa nyota Cristiano Ronaldo wa real Madrid huku Leonel Messi wa Barca akiwa na hatihati baada baada ya kutoka kwenye majeruhi ya goti.
Mbali na mhezo wa El Clasico kutaigwa micheo mingine ya ligi hii
Real Sociedad na Sevilla
Espanyol na Malaga
Valencia na Las Palmas
Posted by Unknown on 20:54:00
with No comments so far
![](http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/11/19/151119114338_manuel_valls_512x288_epa_nocredit.jpg)
Ameyasema hayo wakati alipokuwa anazungumza katika runinga ya taifa hilo na kwamba wahusika wengine wa ugaidi walikuwemo katika nchi za Ufaransa na Ubelgiji mapema.
Waziri huyo aliongeza kuwa haikufahamika mara moja kwamba kulikuwa na makundi ya namna hiyo kwa ukubwa wake ,ama mshukiwa Salah Abdeslam, ambaye ndiye hasa kielelezo cha mwanamume anayesakwa zaidi kimataifa na haikujulikana kama alikuwa Ubelgiji ama Ufaransa.
Posted by Unknown on 07:34:00
with No comments so far
![](http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/10/29/151029023855_south_sudan_624x351_afp_nocredit.jpg)
Kulingana na Mwandishi mmoja katika eneo hilo Philip Thon,kisa hicho kilitokea mwendo wa saa moja katika eneo la Moli yapata kilomita 50 kutoka mji wa mpakani wa Nimule.
Maafisa wa Polisi wa Sudan Kusini wanajaribu kutafuta idadi kamili ya watu waliojeruhiwa.
Watu wanne waliofariki na wengine wanne waliojeruhiwa wamepelekwa katika hospitali ya Juba.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa huenda takriban watu 25 wameuwawa huku wengine wakiwa hawajulikani waliko.
Mwandishi wa BBC Patience Atuhaire mjini Kampala amezungumza na kamanda wa polisi wa jimbo la Kaskazini mwa Uganda ,karibu na mpaka na Sudan Kusini.
Amesema kuwa maafisa wake wanakutana na kujadiliana na wenzao wa Uganda ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Amesema kuwa wanajaribu kutafuta njia ya kuwasafirisha waliojeruhiwa katika hospitali ya Lacor huko Gulu nchini Uganda.
Amekadiria kwamba takriban watu 69 walikuwa wakiabiri basi hilo.
Patience kwa sasa anajaribu kuitafuta kampuni ya basi hilo kwa jina Friendship.
Haijabainika ni nani aliyeshambulia lakini baadhi ya waliojeruhiwa ambao walizungumza na waandishi ,wanasema washambuliaji walikuwa wamevalia sare za jeshi la Sudan Kusini na walikuwa wakizungumza lugha ya eneo hilo.
Biashara imenoga kati ya Kampala na Juba ambapo mabasi na malori yanatumia barabara hiyo.
Ni mara ya kwanza kwa basi la abiria linalotumia barabara hiyo kuvamiwa katika kipindi cha siku za hivi karibuni.
Posted by Unknown on 07:26:00
with No comments so far
![](http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/11/19/151119080535_majaliwa_kassim_512x288_bbc_nocredit.jpg)
Bw Majaliwa amepata kura 258 kati ya 351 zilizopigwa, baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kutangazia bunge kwamba ndiye aliyekuwa amependekezwa na Rais John Pombe Magufuli awe Waziri Mkuu.
Bw Majaliwa, 55, amekuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa, Jimbo la Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) tangu 2010.
![](http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/624/amz/worldservice/live/assets/images/2015/11/19/151119072946_ruangwa_constituency_512x288_bbc_nocredit.jpg)
Alikuwa naibu waziri katika afisi ya Waziri Mkuu aliyehusika na utawala wa mikoa na serikali za mitaa katika serikali ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Anatarajiwa kuapishwa kesho katika ikulu ya Dodoma.
Bw Majaliwa, ambaye ni mwalimu kitaaluma, atamrithi Mizengo Pinda ambaye alihudumu kama Waziri Mkuu chini ya Rais mstaafu Kikwete kuanzia 2008.
Wednesday, 18 November 2015
Posted by Unknown on 19:32:00
with No comments so far
Subscribe to:
Posts (Atom)