![](http://www.tbc.go.tz/image.php?path=news_images/5690MIHAYO%20MSIKHELA.jpg&width=600)
![](http://www.tbc.go.tz/layout/camera.png)
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la KUTIBA AMANI mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa kijiji cha LUEGU wilaya ya NAMTUMBO mkoani RUVUMA, amekutwa amefariki dunia na mwili wake kuharibika baada kufukiwa na kifusi katika shimo ambalo alikuwa akichimba madini aina ya VITO katika machimbo ya MTWARA-PACHANI Wilayani humo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa RUVUMA, MIHAYO MSIKHELA amesema mtu huyo aliondoka nyumbani kwake wiki mbili zilizopita, kwenda katika machimbo yaliyopo MTWARA PACHANI wilaya ya NAMTUMBO Mkoani humo,kwa lengo la kuchimba madini.
kwa upande wake Afisa madini kanda ya ziwa nyasa GEORGE WANDIBHA amesema wameshatoa elimu kwa wachimbaji kuwajulisha juu ya uchimbaji salama na utunzaji wa mazingira na kuwataka kwenda ofisini kuomba leseni lakini hakuna mchimbaji yoyote aliyekwisha omba leseni ya uchimbaji wa eneo hilo
0 comments:
Post a Comment