Kauli hiyo ya Mayweather ni ya kejeli kwa Pacquiao ambaye alimchukia tangu alipotangaza kuwa alipigana na Mayweather akiwa na maumivu ya bega kitu kilichomuudhi Floyd aliyeamini Manny Pacquiao analeta visingizio badala ya kukubali matokeo.
Bondia Floyd Mayweather atapanda ulingoni tarehe 12 mwezi huu kupambana na Mmarekani mwenza Andre Berto katika pambano lake la mwisho la career yake ya ngumi na kama akishinda basi atakua ameweka rekodi ya aina yake ya kutopoteza hata mchezo mmoja kwani hadi sasa ameshinda michezo yote 48 aliyocheza.
0 comments:
Post a Comment