Saturday, 19 September 2015

 
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia wananchi Bukoba waliofika kwenye Mkutano wa Kampeni, kusikiliza sera zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa AghaKhan, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera leo Septemba 19, 2015.
Umati wa Wananchi wa Mji wa Bukoba ukiwa umefurika kwenye Uwanja wa Aghakhan kuhudhulia Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, leo Septemba 19, 2015.
Tanzania imeisimamisha Malawi isiteketeze moto tani 2.6 ya pembe ya ndovu ilizonasa katika operesheni dhidi ya wawindaji haramu
Shehena hiyo ya meno 800 ya ndovu ilinaswa na maafisa wa forodha wa Malawi ilipokuwa ikiingizwa nchini Malawi.
Tanzania ilikimbia mahakamani ilikuizuia serikali ya Malawi isiharibu ushahidi wake dhidi ya watuhumiwa waliokamatwa na kesi inaendelea.Mkurugenzi mkuu wa idara ya kuwalinda wanyama pori wa Malawi anasema kuwa inasikitisha mno kuwa Tanzania imekwenda mahakamani kuizuia idara yake isiteketeza bidhaa hizo haramu kwa miezi mitatu ijayo.
''Tulikuwa tayari kuchoma moto pembe hizo za ndovu ambayo ingekuwa ishara kamili kuwa tunapanga mikakati kabambe ya kupambana na walanguzi na wawindaji haramu ili kulinda ndovu wetu,''''Sasa hilo halitawezekana kwa sasa na hadi baada ya miezi mitatu ijayo'' alifoka Bright Kumchedwa
Idadi ya ndovu imepungua kwa asilimia 50% tangu mwaka wa 1980 nchini Malawi kutokana na uwindaji haramu.
Nchini Tanzania Idadi ya ndovu imepungua kwa asilimia 60% katika kipindi cha miaka mitano tu iliyopita.
Mwezi uliopita mahakama moja iliwapata na hatia kaka wawili raia wa Malawi na hatia ya uwindaji haramu na ulanguzi wa pembe za ndovu.Wawili hao walipigwa faini ya dola elfu tano za Marekani $5,500 na mahakama ikaamuru bidhaa hiyo ichomwe moto katika kipindi cha siku 20.
Lakini serikali ya Tanzania nayo ikakimbia mahakamani ilikuzuia serikali ya Malawi isiteketeza pembe hizo ikidai kuwa itakosa ushahidi wowote dhidi ya watuhumiwa wake wa uwindaji haramu.
Tatizo la uwindaji haramu umekithiri katika miaka ya hivi karibuni kufuatia utashi mkubwa wa bidhaa hiyo inayoenzia katika mataifa ya mashariki ya mbali na bara Asia.Si aghalabu kushuhudia familia nzima ya ndovu na faru wakiangamizwa katika mbuga za wanyama pori barani Afrika ambako ndovu bado wapo.
Mwaka uliopita viongozi wa mataifa ya Botswana, Gabon, Chad na Tanzania yaliafikiana kuthibiti uuzaji wa pembe za ndovu.

Thursday, 17 September 2015


Luke Shaw (kushoto) wakati alipokutana na Hector Moreno kwenye tukio lilipelekea kuvunjika mguu wake wa kulia

Luke Shaw (kushoto) wakati alipokutana na Hector Moreno kwenye tukio lilipelekea kuvunjika mguu wake wa kulia
Klabu ya Man Utd imethibitisha taarifa za Luke Shaw kufanyia upasuaji akiwa nchini Uholanzi baada ya kuvunjika mguu kwenye mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya usiku wa kuamkia jana.

Man Utd imeeleza kwamba, beki huyo mwenye umri wa miaka 20, alilazimika kuachwa nchini Uholanzi kwa matibabu na tayari amefanyiwa upasuaji kwa mafanikio makubwa.
Taarifa zinaeleza kwamba Shaw ataendelea kubaki mjini Eindhoven kwa matibabu mpaka hapo atakaporuhusiwa kurejea nchini England, na kuendelea na mapumziko ya kuuguza jeraha la mguu wake wa kulia.

Huu ndio muonekeno wa mguu wa Luke Shaw mara baada ya kufanyiwa upasuaji uliomalizika salama
Huu ndio muonekeno wa mguu wa Luke Shaw mara baada ya kufanyiwa upasuaji uliomalizika salama
Kabla ya taarifa za klabu kutolewa kupitia tovuti maalum, meneja Louis Van Gaal alinukuliwa na vyombo vya habari akisema Luke Shaw alipangiwa kurejea nchini England kwa ajili ya ufanyiwa taratibu zote za matibabu yake.
Kutokana na ukumbwa wa jeraha la Luke Shaw, inahisiwa huenda beki huyo akawa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi sita.
Mashirika ya misaada yanasema watu robo ya milioni wanaathirika kutokana na ukame katika eneo lililojitangazia uhuru la Somaliland.
Mashirika hayo yanasema utapia mlo umeathiri watu vibaya hasa watoto wa chini ya miaka mitano. Watu kumi na watatu wameripotiwa kufa.
Kulingana na mashirika hayo asilimia arobaini ya mifugo imekufa kutokana na ukosefu wa maji na uhaba wa chakula.
Familia zinalazimika kuishi bila vyakula vya kutosha , kunywa maji machafu na kuhamahama kutafuta chakula.
Maeneo yalioathirika zaidi ni yale ambayo huzalisha chakula kwa kiwango kikubwa.
GIlbert DiendereImage copyright
Image captionDiendere ametetea mapinduzi ya serikali yaliyotekelezwa na walinzi wa rais
Mshirika wa karibu wa rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaore ametangazwa kuwa kiongozi mpya wa taifa hilo na walinzi wa rais kutwaa uongozi waliotwaa mamlaka.
Taarifa iliyotolewa na walinzi hao imesema Jenerali Gilbert Diendere, aliyekuwa mkuu wa majeshi chini ya Compaore, ndiye atakayekuwa rais mpya.
Tangazo la awali kupitia runinga ya taifa lilisema mashauriano yangefanyika kuunda serikali mpya ya mpito ambayo ingeandaa “uchaguzi wa amani na wa kuhusisha wote”.
Spika wa bunge la mpito Cheriff Sy amesema hayo ni “mapinduzi ya serikali”.
Hayo yamejiri huku ufyatulianaji wa risasi ukiripotiwa jiji kuu la Ouagadougou.
Rais Francois Hollande alishutumu hatua ya walinzi hao wa rais ya kupindua serikali.
Walinzi hao wanadaiwa kufyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakiandamana Ouagadougou kupinga hatua ya wanajeshi hao na baadhi wamekamatwa, ripoti zinasema.
Wametangaza amri ya kutotoka nje kote nchini humo, na kufunga mipaka ya taifa hilo, shirika la habari la AFP limeripoti.
Maandamano Burkina FasoImage copyrights
Image captionWatu wamekuwa wakiandamana Ouagadougou kupinga hatua ya walinzi wa rais kuchukua mamlaka
Makao makuu ya chama cha Compaore cha Congress for Democracy and Progress (CDP) yalivamiwa na waandamanaji na kuporwa, baada ya habari za mapinduzi hayo kuenea.
Bw Hollande ameitisha kuachiliwa mara moja kwa Kaimu Rais Michel Kafando na Waziri Mkuu Isaac Zida, waliozuiliwa wakiongoza mkutano wa baraza la mawaziri ikulu ya rais Jumatano.
Serikali yao ya mpito ilitarajiwa kukabidhi mamlaka kwa serikali ambayo ingechaguliwa kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 11.
Bw Compaore aliondolewa madarakani baada ya maandamano ya raia mwaka jana na kwa sasa anaishi uhamishoni. Alikuwa ameongoza taifa hilo kwa miaka 27.
Baadhi ya washirika wake wakuu wamezuiwa kushiriki uchaguzi mkuu huo.
Image copyright
Image captionSudan Kusini
Takriban watu 170 wameuawa baada ya lori la mafuta kulipuka Sudan Kusini kulingana na msemaji wa rais.
Lori hilo lilikosa mwelekeo na kutoka kando ya barabara katika eneo la Maridi,magharibi mwa jimbo la Equitorial kabla ya raia kuanza kufyonza mafuta wakati lilipolipuka alisema Ateny Wek Ateny.
Takriban watu 59 wanadaiwa kujeruhiwa.
Hospitali katika eneo hilo zimezidiwa majeruhi na maafisa wa serikali wameliomba shirika la msalaba mwekundu na umoja wa mataifa kutoa usaidizi.
Lori hilo lilikuwa likisafiri kutoka mji mkuu Juba kelekea Maridi,umbali wa kilomita 250 lilipokosa mwelekeo.
Wakaazi wa jamii zilizopo karibu walifanya kama wanavyofanya raia wengine Afrika kwa kufyonza mafuta kabla ya kupotea.
Waziri wa habari nchini humo Charles Kisagna ameiambia Reuters anahofu kuhusu wale waliojeruhiwa.
Image copyrRA
Image captionAhmed Mohamed
Polisi wa Texas wamemuondolea mashtaka mvulana mwislamu mwenye umri wa miaka 14 aliyekamatwa kwa kutengeza saa.
Maafisa katika shule ya upili ya Mac Arthur mjini Irving waliwaita maafisa wa polisi baada ya kudhania kwamba saa hio ilikuwa bomu.
Kukamatwa kwa Ahmed Mohammed kumekosolewa na wengi huku kijana huyo akipata mwaliko katika ikulu ya White House nchini Marekani.
Image copyrightRays
Image captionAhmed na wazazi wake
Ahmed aliwaambia waandishi wa habari kwamba inasikitisha kwamba mwalimu wake alidhania saa hiyo ilikuwa tishio.''Nilitengeza saa ili kumfurahisha mwalimu wangu lakini nilipomuonyesha alidhani ilikuwa tisho kwa maisha yake. Ninasikitishwa kwamba alinidhania vibaya''.
Katika mkutano huohuo na vyombo vya habari,Ahmed amesema kuwa anataka kuihama shule hiyo.
Image copyrightRays
Image captionAhmed akiwa na saa yake
Babaake kijana huyo Mohammed Elhassan Mohamed ambaye anatoka nchini Sudan,alimsifu mwanawe akisema anatengeza kila kitu ndani ya nyumba yao ikiwemo simu ya babaake na tarakilishi.
''Ni kijana mwerevu sana na kwamba alisema anataka ulimwengu umjue''.Mafisa wa polisi hatahivyo wamekana madai ya familia ya Ahmed kwamba alikamatwa kutokana na jina lake.
''Tumekuwa na uhusiano mzuri na jamii ya waislamu'', alisema mkuu wa polisi wa eneo la Irving Larry Boyd siku ya jumatano.''Visa kama hivi hutoa changamoto.Tunataka kukichukulia kisa hiki kama funzo zuri''.
Rais wa Burkina Faso Michael Kafondo amenyang’anywa madaraka ya kuendelea kuiongoza nchi hiyo baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa Taifa hilo Blaise Compaore.Hatua hiyo imekuja baada ya viongozi hao wawili wa Serikali Kafondo pamoja na Waziri Mkuu wake Isaac Zida kuzuiliwa kuingia kwenye mkutano wa Mawaziri na walinzi waliokuwa wa Rais Compare.
Vurugu zilitanda katika mji mkuu wa nchini hiyo Ouagadougou huku risasi zikirushwa hovyo hewani ili kuwatawanya waandamanaji waliojitokeza kwa wingi kupinga rais huyo kuendelea kubaki madarakani.
Shirika la Voice of America limesema Rais huyo, Waziri mkuu pamoja na viongozi wengine wa Serikali waliwekwa chini ya ulinzi na kikosi cha usalama RSP kinachomsapoti Rais aliyeondoka madarakani Blaise Compaore.
Compaore aliondolewa madarakani kwa nguvu ya wananchi Octoba 2014 na kuteuliwa Rais wa mpito kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu October 11 mwaka huu

Wednesday, 16 September 2015














 
Advertisement


Jengo refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati lazinduliwa nchini Tanzania.
PSPF Towers ni moja ya majengo machache marefu barani Afrika na ndiyo jengo refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati, likiwa na urefu wa mita 147.Majengo mengine marefu Afrika ni Carlton Centre (mita 223) lililopo Afrika Kusini, Hassan II Mosque (mita 210) lililopo Moroko, Ponte City (mita 173) lililopo Afrika Kusini, Necon House (Mita 160) lililopo Nigeria, Marble Tower (mita 152), Pear dawn (mita 152), Pear dawn (mita 152), Met Life
Centre (mita 150) na 88 on field (mita 147) yote ya Afrika ya kusini.
Jengo hilo lililozinduliwa na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, ujenzi wake ulitumia miaka minne tangu mwaka 2011 hadi 2015 limegharimu shilingi bilioni 139.20 za Tanzania lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88. Pia katika jengo hili kuna sehemu ya mgahawa, mabenki, bwawa la kuogelea, Sehemu za kufanyia mazoezi, maegesho ya magari na sehemu nyingine muhimu.
Kudumu kwa rekodi ya urefu ya PSPF Towers lenye minara miwili na ukubwa wa mita za mraba 73,000, kutategemea kukamilika kwa majengo mengine yanayochipua kwa kasi katika Afrika

Tuesday, 15 September 2015

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi5-puqI7gBoWbCGHJYfvBKs7DpbUGLFoyOwwK7hGpIToxvhKCBl4_3eAWo9i4s1UOQ-m4a4eEdQwtoQi3cPgK8_U4AfvOrpggyaDHYNYLryXBt2SxJcxCUEIunvJ-FLoGKcPDnc4YG-siX/s1600/WP_20150916_016.jpg