Thursday, 10 December 2015

Chuo kikuu cha John HopkinsUpasuaji umepangwa kufanyika kwa mara ya kwanza kupandikiza uume nchini Marekani, kwa lengo la kuwasaidia mpiganaji wa zamani
Upasuaji huo wa saa 12- utahusisha ushonaji wa neva muhimu na mishipa ya damu kwa ajili ya kutunza mkojo na kumuwezesha mgonjwa kufanya tendo la ngono.
Upasuaji huu unafuatia mafanikio ya kwanza kabisa ya upandikizaji wa uume nchini Afrika kusini mwaka jana.
Jopo la madaktari kutoka Hospitali ya chuo kikuu cha Hopkins (JHU) wanapanga kumfanyia upasuaji huyo mwanajeshi wa zamani mwenye umri wa miaka 60kama sehemu ya majaribio.
Upasuaji wenyewe
Hatua ya kwanza ya upasuaji huo itaanza kwa kuondoa uume kutoka kwa kijana aliefariki ambaye alijitolea kutoa uume wake kwa ruhusa ya familia yake.
Kwa mujibu wa jopo la madakatari katika JHU matumaini ya mwanajeshi huyo wa zamani ni kwamba hisia za uume wake zitarejea katika muda wa miezi 12.
Uwezekano wa mgonjwa kupata watoto, utategemea kiwango cha jeraha na mafanikio ya upasuaji huo.
Lakini Wanasayansi wanasema kutokana na kwamba ni upasuaji mmoja wa kupandikiza uume uliofanyika, madaktari watakua makini kuhakikisha kuna matumaini ya kweli.
KirchnerCristina Fernandez de Kirchner anayeondoka madarakani Argentina amesusia hafla ya kumkabidhi mamlaka mrithi wake Mauricio Macri.
Kiongozi huyo ametofautiana na mrithi wake kuhusu ni wapi hafla hiyo inafaa kuandaliwa.
Bi Fernandez aliwaaga raia kwenye mkutano mkubwa wa wafuasi wake jana ambapo alitoa hotuba yenye hisia tele hisia nje ya ikulu Jumatano.
Alivishutumu vyombo vya habari vya nchi hiyo kwa kuipiga vita serikali yake ya mrengo wa kushoto.
Aliwahimiza raia kuandamana barabarani iwapo watahisi kusalitiwa na serikali mpya inayoegemea siasa za mrengo wa kati-kulia.
Bw Macri tayari amewasili katika majengo ya Bunge akifuata msafara wa polisi na wanajeshi wenye kupanda farasi. Msafara wake uliwapita mamia ya maelgu ya watu waliojitokeza katika barabara za mji mkuu Buenos Aires.
Atakula kiapo mbele ya wabunge mwendo was aa sita saa za Argentina.
Baada ya hotuba yake ya kwanza, atasafiri hadi ikulu ya rais ambako atapokezwa ishara na nembo za urais.
Bi Fernandez alikuwa amesisitiza shughuli ya kukabidhi madaraka ifanyike mbele ya Bunge, ambako chama chake kina wingi wa viti.
Alisema yeye pamoja na mumewe ambaye ni mtangulizi wake, Nestor Kirchner, walipokezwa ishara na nembo za urais huko na hivyo basi hilo linafaa kuendelezwa.
Bw Macri kwa upande wake anasema kwa mujibu wa itifaki, hafla ya kupokezwa mamlaka inafaa kufanyika ikulu ya rais, kama ilivyokuwa kabla ya 2003.
KasiJeshi la wanahewa la Afrika Kusini limesema duma wawili, ambao hufugwa kwenye kambi ya jeshi hilo ili kufukuza wanyama wengine njia ya kutumiwa na ndege kupaa, wamemshambulia afisa wa jeshi.
Msemaji wa jeshi hilo Marthie Visser amesema kupitia taarifa kwamba duma hao waliingia eneo ambalo ndege huegeshwa katika eneo la Makhado.
Mwanajeshi aliyekuwa kwenye zamu aliwaona na kujaribu kuwapiga picha na hapo ndipo wakamshambulia.
Mwanajeshi huyo hakujeruhiwa vibaya na ameachiliwa kutoka hospitalini.
Wanyama hao hawatafukuzwa katika kambi hiyo.
Bi Visser alisema kambi hiyo, iliyo kaskazini mwa Afrika Kusini, imezingirwa na mbuga za wanyama na duma hao husaidia kudhibiti ongezeko la wanyama mwitu.
BARAZA LA MAWAZIRI

Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri - George Simbachakene  na Angella Kairuki
Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri - Jenista Muhagama
MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri - Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri - William Ole Nasha

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani

Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri - Ashantu Kizachi

Wizara ya Nishati na Madini
Waziri - Prof. Mwigalumi Muhongo.
Naibu Waziri - Medalled Karemaligo.

Wizara ya Katiba na Sheria,
Waziri - Harrison Mwakyembe

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri - Dk. Augustino Mahiga
Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri - Dk. Hussein Mwinyi

Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri - Charles Kitwanga.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri - William Lukuvi
Naibu Waziri - Angelina Mabula

Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Charles Mwijage.

Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi.
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri - Ummy Mwalim
Naibu Waziri –  Dkt. Hamis Kigwangala

Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri - Nape Nnauye
Naibu Waziri - Anastasia Wambura.

Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Prof. Makame Mbarawa
Naibu  Waziri– Inj. Isack Kamwela

Wednesday, 9 December 2015














Mgogoro wa mamilioni ya fedha yaliyokuwa yakidaiwa katika madai ya kesi ya haki miliki ya wimbo wenye umaarufu mkubwa duniani wa 'happy birthday' umetatuliwa kabla kesi hiyo haijatolewa hukumu huko Los Angeles nchini Marekani.
Kampuni ya kurekodi muziki ya Warner Chappel, imesema ilinunua haki miliki ya wimbo huo mnamo mwaka 1935, lakini mwanzoni mwa mwaka huu hakimu anayesimamia kesi hii, alisema wimbo huo hauna haki miliki ya kuwa na mashairi yenye lugha ya kiingereza.
Wanamuziki na watengeneza filamu wametakiwa kulipia dola milioni mbili kwa mwaka kama gharama ya kuutumia wimbo huo kwa umma kwa mwaka. Ingawa vigezo vyake bado havijawekwa wazi.
GiroudOlivier Giroud alifungia Arsenal mabao matatu kwa mara yake ya kwanza na kuhakikisha Gunners wanaendeleza rekodi yao nzuri Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na kufika hatua ya 16 bora kwa kulaza Olympiakos.
Arsenal walihitaji kushinda kwa mabao mawili wazi lakini walipata mabao hata zaidi na kumaliza wa pili Kundi F.
Giroud alianza kwa kufunga kwa kichwa kipindi cha kwanza, kisha akafunga la pili kipindi cha pili kwa usaidizi kutoka kwa Joel Campbell.
Mfaransa huyo alihakikisha Arsenal wanafuzu kwa kufunga la tatu kupitia penalti.
Arsenal hawajawahi kukosa kufika hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya tangu kuanza kwa mfumo wa sasa 2003-4, na walionyesha uzofu wa kusakata gozi katika jukwaa kuu Ulaya kwa kung’aa Athens.
Takwimu muhimu:
  • Olivier Giroud ndiye mchezaji wa nne kufungia Arsenal hat-trick kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (baada ya Thierry Henry, Nicklas Bendtner na Danny Welbeck).
  • Vijana wa Arsene Wenger wameshinda mechi yao ya kwanza Ugiriki tangu Desemba 1998 (3-1 dhidi ya Panathinaikos).
  • Giroud ndiye mchezaji was aba wa Arsenal kufikisha magoli kumi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya (wengine wakiwa Henry, van Persie, Ljungberg, Fabregas, Walcott na Pires the others).
  • Matokeo ya Jumatano yalifikisha kikomo msururu wa kutoshindwa wa Olympiakos wa mechi sita katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya timu za Uingereza(Kushinda 5, Sare 1)
  • Arsenal walikuwa wameshindwa mechi tatu zao za awali ugenini dhidi ya Olympiakos zote katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, zote katika mechi ya sita hatua ya makundi.
Matokeo kamili ya mechi za UEFA zilizochezwa Jumatano:
  • Bayer Leverkusen 1 - 1 Barcelona
  • Olympiakos 0 - 3 Arsenal
  • Chelsea 2 - 0 FC Porto
  • Valencia 0 - 2 Lyon
  • Roma 0 - 0 BATE Borisov
  • Dinamo Zagreb 0 - 2 Bayern Munich
  • Dynamo Kiev 1 - 0 M'bi Tel-Aviv
  • KAA Gent 2 - 1 Zenit St Petersburg
Bosi wa Manchester United Louis van Gaal amesema hana kisingizio chochote cha kwanini wametolewa kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, na sasa kucheza UEFA EUROPA LIGI.
Hii ni mara ya 4 kwa Man United kushindwa kuvuka hatua ya Makundi ya UCL baada ya Jana kuchapwa 3-2 na Wolfsburg na kushushwa Nafasi ya 3 ya Kundi B na hivyo kucheza Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya UEFA EUROPA LIGI.
Licha ya kushindwa kuvuka toka Kundi B ambalo Wachambuzi walihisi kuwa ni jepesi kwani Timu nyingine zilikuwa PSV Eindhoven na CSKA Moscow, Louis van Gaal amesisitiza Man United iko kwenye njia sahihi chini yake.
United iko katika nafasi ya nne katika Ligi Kuu, wakiwa walimaliza katika nafasi kama hiyo katika msimu wa kwanza wa Van Gaal.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mtaro wa maji machafu kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitoka eneo la shimoni kwenye soko kuu la Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
 Waziri Mkuu,Kassim Majliwa akiwa amezongwa na wananchi wakati alipokwenda kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam kufanya usafi Desemba 9, 2015.
Baadhi ya washiriki wa zoezi la usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam wakipiga picha kwa kutumia simu wakati Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa alipozunguza nao baada ya kufanya usafi sokoni hapo Desemba 9, 2015.
 Gari alilopanda Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa likitoka kwenye eneo la soko kuu la Kariakoo alikokwenda kushiriki katika kufanya usafi Desemba 9, 2015.
 HAPA KAZI TU ya  Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe  Joseph Magufuli  ikiendelea kufanyiwa kazi kama Rais  huyo akionekana katika picha akiwa sambamba na mkewe Mama Janeth Magufuli,wakishiriki kufanya usafi leo ndani na nje viunga vya Ikulu ikiwemo pia soko la Samaki Feri,ambako alipata wasaa kuwasikiliza wachuuzi wa samaki na wavuvi.
guf1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mama Janeth Magufuli wakielekea eneo la ufukwe wa Ferry kufanya usafi katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru tarehe 9 Desemba.
guf2 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizoa taka katika eneo la ferry jijini Dar es Salaam.
guf3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizoa taka katika eneo la ferry jijini Dar es Salaam.
guf7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka taka ndani ya ndoo ya Taka katika eneo la Magogoni jijini Dar es Salaam.
guf8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiwa pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakifanya usafi katika eneo la ufukwe wa ferry jijini Dar es Salaam.
guf9guf10 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka taka taka kwenye dastibin wakati akifanya zoezi la kufanya usafi katika eneo la ufukwe wa Ferry jijini Dar es Salaam.
guf11 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiokota takataka katika eneo la Ferry katika zoezi la kufanya usafi nchi nzima.
guf12 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiokota takataka katika eneo la Ferry katika zoezi la kufanya usafi nchi nzima.
guf13 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wavuvi wa ferry huku akiwa ndani ya Mtumbwi. Rais Magufuli alizisikiliza kero zao na kuahidi kuzitatua ndani ya muda mfupi.guf14 
Rais Magufuli akifanya usafi pamoja na wavuvi wa eneo la ferry waliojitokeza kuungamkono zoezi hilo. Rais Magufuli amewataka Watanzania kuwa na Utamaduni wa kufanya Usafi kila wakati ili kuweka mazingira katika hali nzuri. PICHA ZOTE NA IKULU