Kulia ni mwanafunzi ambaye alimtoroka mume wake baada ya baba yake mzazi kuamua kumozesha kwa mahali ya ng’ombe 150 kushoto ni mama mlezi Veronica Kilango wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe pamoja na maafisa kutoka shirika la Plan International mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishi wa habari.
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
WAZAZI na walezi hapa nchini wametakiwa kuachana na mila zilizopitwa na wakati kwa kuwaozesha watoto wao mapema hususan wa kike wakiwa katika umri mdogo na kupelekea baadhi yao kukatisha masomo yao na badala yake wawe na mawazo chanya ya kuwasaidia katika kuwalinda na kuwapatia haki zao za msingi katika elimu.
Kauli hiyo imetolewa na mwanafunzi mmoja anayesoma kwa sasa kidato cha tatu ambaye jina lake linahifadhiwa kutokana na kulinda haki za watoto wakati wa ziara ya siku mbili Wilayani Kisarawe Mkoa wa Pwani iliyofanywa na shirikika la kimaendeleo linalojishughulisha na kutoa misaada kwa binadamu Plan International kwa lengo la kubaini changamoto zinazowakabili watoto.
Mwanafunzi huyo akizungumza kwa majonzi na waandishi wa habari pamoja na watendaji wa halmashauri ya Kisarawe pamoja na watumishi wa Plan international amesema kwamba amesikiteshwa sana kuona wazazi wake wanamkatisha masomo yake na kumwozesha kwa nguvu bila lidhaa yake kwa mwanaume.
Aidha binti huyo amebainisha kuwa baada ya mwaka 2014 mwanzoni kumkatalia baba yake mzazi kuolewa ndipo mazi wake alipoamua kutumia njia nyingine ya kumdang’anya anamtafutia uhamisho wa kwenda kusomea shule nyingine iliyopo Wilayani Mkuranga kumbe alikuwa tayari amemtafutia mwanaume kwa nguvu kwa lengo la kumwozesha mwanae.
Akielezea zaidi kuhusiana na tukio hilo mwanafunzi huyo baada ya baba yake kumwozesha kwa mwanaume huyo alikwenda kusihi nae kwa kipindi cha miezi miwli na baada ya hapo aliweza kumtoroka na kukimbilia katika Wilaya ya Kisarawe ambapo alimpata msamalia mwema ambaye anaishi nae kwa sasa.
“Kwa kweli mimi msichana mdogo lakini kwa kitendo ambacho alinifanyia baba yangu kwa kuamua kunilazimisha kuolewa kwa mabadilishano ya ng’ombe 150 nimesikitisikitika sana na mimi napenda sana masomo, hivyo wakati nipo naishi na huyo mwanaume nilikutana na mtu mmoja nikwamwelezea akakubali kunisaidia na ndipo nilipoamua kumtoroka na kwenda Kisarawe.”alisema Mwanafunzi huyo kwa uchungu.
Kwa upande wake Afisa ustawi wa Jamii Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani amethibitisha kutokea kwa taarifa za tukio hilo la mwanafunzi na kwamba wamempokea na kumpatia msaada wa hali na mali ikiwemo kumpatia mahitaji muhimu na kumpeleka shule ambapo kwa sasa anaendelea na masomo.
Kwa upande wake mmoja wa mjumbe wa kamati ya ulinzi ya mtoto Wilaya ya Kisarawe Saimon Mpunga akizungumza kwa niaba ya wajumbe wenzake amesema kwamba kuja haja ya kuwafichua wazazi wenye tabia kama hizo na kuongeza kuwa baada ya mradi huo wa wa kupinga ukatili dhidi ya watoto kuanziashwa na Plan International jamii imeweza kuvunja ukimya.
Mwandishi wa habari hizi aliweza kupata fursa ya kuzungumza na mama mlezi ambaye anamlea mwanafuzni huyo kwa sasa aliyejitambulisha kwa jina la Veronica Kilango ambaye alisema kwa sasa mwanafunzi huyo aliamua kumsaidia kwa hali na mali na kwamba kwa sasa aneendelea na masomo yake katika shule moja ya sekondari iliyopo wilayani Kisarawe.
Aidha Kilango alitoa wito kwa jamii na wazazi kuhakikisha kwamba wanaachana na vitendo vya unyanyasaji na ukatili kwa watoto wadogo na badala yake wabadilike na kuhakikisha wanawalinda na kuwapatia haki zao za msingi ikiwemo kuwaendeleza kimasomo na sio kuwakatisha kwa kuwaozesha.
Naye Mratibu wa Mradi wa kupinga ukatili kwa watoto kutoka Shirika la Plan International, Neema Daniel alisema kwamba kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na jamii kutokuwa na mwamko mkubwa wa kutoa taarifa ya kuwafichua watu wanaohusika na vitendo hivyo vya ukatili kwa watoto wadogo.
Kuanzishwa kwa Mradi huo wa Plan International wa kupinga ukatili dhidi ya watoto umeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa na kufanikiwa kumpata na kumsaidia mwanafunzi huyo ambaye aliozeshwa na baba yake mzazi kwa mwanaume mwenye umri wa mika (30) kwa ng’ombe 150
0 comments:
Post a Comment