Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli(katikati) akiwanadi Mbunge wa Handeni Mjini Dk. Abdallah Kigoda (kulia) na Mgombea wa Ubunge Jimbo la Handeni Vijijini Ndugu Mboni Mhita kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uliofanyika kwenye uwanja wa Azimio Center.
Mzee Yusuph Makamba akihutubia wakazi wa Turiani mkoani Morogoro kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa CCM pamoja na sera za CCM kwa wananchi wa Turiani.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuliambapo aliwaambia wananchi hao ataunda baraza dogo la mawaziri lakini pia atahakikisha barabara zinakamilika kwa kiwango cha Lami.
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Songe ambapo aliwaambia wananchi hao katika uongozi wake atasimamia haki kwa wananchi wote na kuhakiisha huduma zote za msingi zinapatikana.
Msafara wa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili Kwediboma.
Wananchi wa Handeni wakishangilia jambo kwenye mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Azimio Center mkoani Tanga
0 comments:
Post a Comment