Monday, 7 September 2015

 Mkuu wa kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, Fredrick Nisajile akiongea na wakimbizi walio katika mpango wa kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Mtendeli na Karago.Wakimbizi hao waliopokelewa kutoka nchini Burundi hivi karibuni kwa sasa wanahifadhiwa kwa muda katika kambi ya Nyarugusu.
 Wakimbizi kutoka nchini Burundi wakipanga mizigo yao katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wamehifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Karago na Mtendeli ikiwa ni mkakati unaoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengine ya kimataifa ili kuwapatia makazi salama
Categories:

0 comments:

Post a Comment