Friday, 18 March 2016

SimbaSimba aliyetoka katika mbuga ya taifa ya wanyama ya Nairobi amemshambulia mzee mmoja jijini humo mapema asubuhi.
Simba huyo alitoka mbugani na kuonekana karibu na eneo la City Cabanas, katika ya Mombasa Road.
Afisa wa mawasiliano wa Shirika la Huduma kwa Wanyamapori (KWS) Bw Paul Udoto ameambia BBC kwamba mzee aliyejeruhiwa ni wa umri wa miaka 63 na amepewa matibabu ya dharura katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kisha akakimbizwa hospitalini kwa matibabu kamili.
Hata hivyo, Bw Udoto amesema mzee huyo hayuko hatarini.
Kwa mujibu wa afisa huyo, simba huyo huenda alikerwa na kelele za magari yaliyokuwa yakipita.
Vikosi vitatu vya maafisa wa KWS vilitumwa kumdhibiti na kwa mujibu wa Bw Udoto, simba huyo anaelekezwa ndani kwenye mbuga.
Maafisa wanaendelea kushika doria kubaini iwapo kuna simba wengine walitoka mbugani.
Visa vya simba kutoka mbugani vimekuwa vikiripotiwa siku za karibuni. Mwezi mmoja uliopita, simba wanne waliingia maeneo ya makazi eneo la Langata.
Wiki mbili zilizopita, simba wawili walidaiwa kuonekana karibu na barabara ya Ngong.
HABARI KWA NIABA YA BBC SWAHILI.





Tuesday, 15 March 2016


Ndovu mmoja kwa jina Morgan amefanikiwa kuvuka mpaka na kuingia nchini Somalia mwezi huu, na kuwa mara ya kwanza ndovu huyo kuonekana nchini humo tangu miaka 20 iliyopita.
Ndovu huyo kwa jina Morgan aliye na umri wa takriban miaka 30, alifungiwa kifaa ya kufuatilia mienendo yake mwezi Disemba katika eneo la Tana River pwani mwa kenya, kati kati ya mwezi Februari kabla ya kuanza safari isiyotarajiwa kuelekea nchini Somalia na kufanikiwa kuwasili mpakani wiki tatu baadaye.
Safari yake imewashangaza watunza mazingira ambao wanasema kuwa hatua hiyo inaonyesha kuwa ndovu huyo alikumbuka njia za zamani baada ya miongo kadha ya kuondoka Somalia kutokana na mapigano.
Safari ya Morgan ni ishara tosha kuwa eneo la mpaka kati ya Kenya na Somalia, linaonekana kuboreka kiusalama na ikiwa hali itakuwa shwari kusini mwa Somalia, basi ndovu waishio uhamishoni watarudi nyumbani.
Kutoka ene la Tana River Morgan alitembea umbali wa kilomita ishirini usiku wa kwanza kabla ya kujificha ndani ya msitu mkubwa na kuendelea na safari siku iliyofuata . Alirudia mtindo huo kwa siku 18.

Serikali ya Sudan Kusini imefeli kubatilisha uamuzi wa mahakama unaoishtumu kwa kukataa kumkamata rais wa Sudan Omal al- Bashir wakati alipohudhuria mkutano wa AU mnamno mwezi juni.
Kushindwa kwa serikali kutekeleza agizo la kumkamata lililotolewa na mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC ni kinyume na sheria za taifa hilo,mahakama ya rufaa iliamuru.
Mahakama ya chini ilitoa uamuzi kama huo,na serikali ina matumaini kwamba itashinda rufaa.
Inahoji kwamba Bashir ana haki ya kinga ya kirais.
Urusi
Wanajeshi wa Urusi wameanza kuondoka Syria siku moja baada ya Rais Vladimir Putin kushangaza wengi kwa kutangaza kwamba wanajeshi wa nchi yake wangeondoka nchini humo.
Kundi la kwanza la ndege za kivita za nchi hiyo limeondoka kutoka kambi ya Hmeimim nchini Syria mapema asubuhi, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema.
Mataifa ya Magharibi yamefurahia hatua hiyo, ingawa kwa tahadhari, yakisema itaishinikiza serikali ya Syria kushiriki kwenye mazungumzo.
Mazungumzo ya amani yanayolenga kumaliza mzozo nchini humo yameingia siku yake ya pili leo.
Hayo yakijiri, tume ya Umoja wa Mataifa inatarajiwa kutoa ripoti ya kutekelezwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita nchini Syria baadaye leo.
Hatua ya kuondolewa kwa baadhi ya wanajeshi wa Urusi nchini Syria ilitangazwa Jumatatu wakati wa mkutano kati ya Bw Putin na mawaziri wake wa ulinzi na mashauri ya kigeni.
Bw Putin alisema majeshi hayo yametimiza lengo lililokusudiwa.Putin
Urusi ni mshirika mkubwa wa Rais wa Syria Bashar al-Assad, na afisi yake imejaribu kuondoa uvumi kwamba kumezuka tofauti baina ya nchi hizo mbili, na kusema uamuzi huo ulifikiwa kwa pamoja.
Operesheni ya kijeshi ya Urusi ilianza Septemba mwaka jana na kuisaidia sana serikali ya Syria ambayo ilifanikiwa kukomboa maeneo kutoka kwa waasi.
Kwa mujibu wa waziri wa ulinzi Sergei Shoigu, kama alivyonukuliwa na vyombo vya habari vya Urusi, ndege za kivita za taifa hilo lilifanya safari 9,000 na kusaidia kukombolewa kwa maeneo 400 ya makazi.
Jeshi la Urusi, amesema Bw Shoigu, lilisaidia serikali ya Bw Assad kukomboa eneo la kilomita mraba 10,000.
Mtawa
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametangaza kwamba Mother Teresa atafanywa mtakatifu Septemba mwaka huu.
Sherehe ya kumtawaza kuwa mtakatifu itafanyika tarehe 4 Septemba.
Njia ya kumfanya mtakatifu ilifunguliwa Desemba mwaka jana baada ya Vatican kutambua muujiza wa pili uliohusishwa naye. Muujiza huo alipokea mwanamme raia wa Brazil ambaye alipona saratani kwenye ubongo wake.
Mother Teresa alipewa tuzo ya amani ya Nobel kutokana na huduma yake kwa raia maskini kwenye vitongoji wa jimbo la Kolkata nchini India.
Alifariki dunia mwaka 1997.Papa

Klabu 5 za Ligi Kuu England Leo zitaingia kwenye Chungu cha kufanyia Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali za EMIRATES FA CUP.
Timu hizo 5 zitakazoshiriki kombe hilo kongwe duniani ni Manchester United, West Ham, Everton, Watford na Crystal Palace, Wakati Everton.
Watford na Crystal Palace tayari zimetinga Nusu Fainali, Man United na West Ham inabidi zirudiane huko Upton katika Tarehe itakayopangwa baadae baada ya Jana Jumapili kwenda Sare 1-1 huko Old Trafford na Mshindi kutinga Nusu Fainali.
Kati ya hizi Timu 5 ni Man United pekee yenye rekodi ya kutwaa Mataji makubwa katika Miaka 20 iliyopita.
Mechi za Nusu Fainali zimepangwa kuchezwa Uwanja wa Wembley Jijini London hapo Jumamosi Aprili 23 na Jumapili Aprili 24.
Fainali ya FA CUP itachezwa pia Uwanjani Wembely hapo Mei 21.
Katika Droo ya Leo, Timu zimepewa Namba za Vipira ambavyo vitawekwa kwenye Chungu, 1 - Crystal Palace, 2 – Everto ,3 – Watford, 4 - West Ham United na Manchester United.
Jedwali la msimamo wa ligi ya EPL kufikia 15 Machi, 2016.

Nambari Klabu Mechi Mabao Alama
1 Leicester 30 22 63
2 Tottenham 30 29 58
3 Arsenal 29 16 52
4 Man City 29 21 51
5 West Ham 29 12 49
6 Man Utd 29 10 47
7 Southampton 30 8 44
8 Liverpool 28 6 44
9 Stoke 30 -4 43
10 Chelsea 29 4 40
11 West Brom 29 -6 39
12 Everton 28 12 38
13 Bournemouth 30 -9 38
14 Watford 29 -1 37
15 Crystal Palace 29 -7 33
16 Swansea 30 -10 33
17 Sunderland 29 -19 25
18 Norwich 30 -23 25
19 Newcastle 29 -26 24
20 Aston Villa 30 -35 16

Michuano ya klabu bingwa barani ulaya inatarajia kuendelea tena leo jumanne kwa Michezo Miwili.
Atletico Madrid yenye pointi 13 watakuwa wenyeji wa Psv Endovein yenye point 10 katika msimamo, na Manchester city yenye alama 12 wao watakuwa nyumbani Etihad wakiwaalika Dianamo Kiev ya Ukrain yanye alama 11 mpaka sasa.
Michuano hiyo itaendelea tena kesho Jumatano kwa mechi mbili, Barcelona watakuwa wenyeji wa Arsenal, na Bayern Mun wataikabili Juventus.
Fainali za Michuano hiyo zitahitimishwa tarehe 28 mwezi Mei 2016 uwanja wa San Siro Milan nchini Italy.
Shinji
Leicester City wamepanua uongozi wao kileleni mwa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kupata ushindi dhidi ya Newcastle.
Lecester walilaza Newcastle, waliokuwa wakicheza mechi yao ya kwanza chini ya meneja mpya Rafael Benitez, kwa bao 1-0 mechi hiyo iliyochezwa Jumatatu usiku.
Shinji Okazaki ndiye aliyewafungia bao hilo la pekee, na alilifunga kwa ustadi wa aina yake dakika ya 25.Shinji
Leicester City sasa wanazidi kukaribia kushinda taji lao la kwanza kabisa la ligi zikiwa zimesalia mechi nane msimu huu.
Newcastle walionekana kuimarika na walikaribia kufunga kupitia Ayoze Perez na Moussa Sissoko lakini bahati yao haikusimama.
Kabla ya mechi hiyo, meneja wa Leciester Claudio Ranieri alikataa kukubali kwamba ndio wanaopigiwa upatu kushinda ligi.
Badala yake, alisisitiza kuwa lengo lao ni kufuzu kwa Europa League.
Vijana hao wa Ranieri kwa sasa wamo alama 12 mbele ya Manchester City na 11 mbele ya Arsenal, jambo linalowafanya wengi kuamini kwamba sasa vita vya kushindania ligi ni kati yao na Tottenham walio nambari mbili.
Kwa Newcastle, mechi mbili zijazo zitakuwa muhimu katika kufufua matumaini yao ya kutaka kusalia ligi kuu.
Watakuwa wenyeji wa Sunderland Jumapili kisha wakutane na Norwich ugenini tarehe 2 Aprili.
Leicester watasafiri kukutana na Crystal Palace Jumamosi.
Mechi zijazo za Leicester City:
Jumamosi 19 Machi 2016Crystal Palace v Leicester 18:00
Jumapili 3 Aprili 2016Leicester v Southampton 16:30
Jumapili 10 Aprili 2016 Sunderland v Leicester 16:30
Jumapili 17 Aprili 2016Leicester v West Ham 16:30
Magufuli
Kampuni inayotarajiwa kufanikisha ujenzi wa bomba la mafuta kutoka bandari ya Tanga hadi nchini Uganda imesema iko tayari kuanza ujenzi huo.
Makamu wa Rais wa kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw Javier Rielo amemwambia Rais wa Tanzania John Magufuli, kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi huo haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.
Mradi huo utahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilometa 1,410 ambalo litasafirisha mafuta ghafi kutoka ziwa Albert nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Utarajiwa kuzalisha ajira za moja kwa moja 1,500 na ajira zisizo za moja kwa moja 20,000.
Bw Javier, akikutana na Rais Magufuli ikulu ya Dar es salaam, amesema kampuni yake inatarajia kutumia dola za kimarekani karibu bilioni 4 ambazo tayari zimeshaandaliwa, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Rais Magufuli ameitaka kampuni hiyo kuharakisha mchakato wa kuanza kwa mradi, na kupendekeza muda wa miaka mitatu uliopangwa kuukamilisha mradi huo upunguzwe, ili manufaa yake yaanze kupatikana mapema.
Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo, Tanzania pia inatarajia kunufaika zaidi na bomba hilo, kwa kuwa kuna tafiti mbili za mafuta zinazoendelea katika ziwa Tanganyika na katikati mwa Tanzania.
Amesema zikikamilika kwa mafanikio, inatarajiwa bomba hilo litasaidia kusafirisha mafuta yake.
Makubaliano ya kujengwa kwa bomba hilo yaliafikiwa wakati wa mkutano kati ya Rais Magufuli na Rais wa Uganda Yoweri Museveni mapema mwezi huu.
Goddard
Mhadhiri mmoja mashuhuri wa somo la kemia katika chuo kimoja kikuu nchini Uingereza amejiuzulu baada ya kugunduliwa kuwa amekuwa akiishi maisha mara mbili.
Amekuwa akifunza kama Profesa na vilevile kuigiza kisiri katika filamu za ngono.
Profesa Nicholas Goddard, ambaye ana umri wa miaka 61, amekuwa akifunza katika Chuo Kikuu cha Manchester kwa miaka 25 na amechapisha vitabu na majarida kadhaa ya kimasomo.
Aligunduliwa na mmoja wa wanafunzi wake baada ya kumtambua katika filamu moja ya uigizaji wa ngono.
Nicholas Goddard, anasemekana kuwa alikuwa akiigiza kwa kutumia jina la utani "Old Nick" kwa zaidi ya miaka kumi.
Aliachana na uigizaji huo mwaka jana wa 2015.
mawaziri
Rais wa Rwanda Paul Kagame amelaumu Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kutumia pesa ‘kiholela’ kutokana na mawaziri kufanya ziara za mara kwa mara kuhudhuria mikutano.
Amesema mawaziri wa nchi yake wanatumia chombo hicho kama njia ya kujinufaisha kwa kufanya ziara na kuhudhuria mikutano ya jumuiya hiyo isiyo muhimu.
Ameahidi kuiga mfano wa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kutokomeza ufisadi huo wa kusitisha ziara za mawaziri alizotaja kuwa za kufuja mali ya taifa.
Akiongea katika mkutano wa faragha wa viongozi wa taasisi zote za serikali nchini Rwanda, Rais Kagame amesema suala la ufisadi nchini humo linachukua mwelekeo mpya na kasi ya ajabu na kwamba hawezi kuendelea kuvumilia.
Rais Kagame aidha amesema Jumuiya ya Afrika Mashariki imeanza kuwa ghali na mzigo kwa taifa lake akisema mawaziri katika mataifa wanachama wanatumia jumuiya hiyo kama chombo cha kuchota pesa kwa kubuni mikutano ya kila siku baadhi akiitaja kuwa haina umuhimu wowote.
Amesema mawaziri wake wasiopungua watano wanasafiri kama mara tatu kwa wiki kushiriki mikutano ya EAC popote inapotokea katika nchi wanachama na kwamba ziara hizo zinaigharimu serikali kitita kikubwa cha pesa.
“Ni kama mawaziri wa nchi hizi walikubaliana kushinikiza serikali zao kuwa lazima wahudhurie kila aina ya vikao vya jumuia hii kwa kisingizio kuwa waziri anayeshindwa kuhudhuria nchi yake inachukuliwa hatua ama inaonekana kupinga juhudi na mikakati ya jumuiya,” amesema Rais Kagame.
Moja ya njia alizosema anaweza kutumia ni kumpa waziri wake wa masuala ya EAC Valentine Rugwabiza jukumu la kushughulikia masuala yote yanayohusu jumuiya hiyo.Magufuli
Amepongeza juhudi za Rais wa Tanzania John Magufuli za kukomesha ufisadi uliokuwa umekithiri katika taasisi za serikali, akisema lazima na yeye afuate nyayo za Rais Magufuli katika suala zima la kukomesha ufisadi na ufujaji wa mali ya serikali.
Rwanda inaorodheshwa ya kwanza katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kupambana na rushwa na ufisadi.
Mwandishi wa BBC Yves Bucyana anasema miaka ya nyuma viongozi kadhaa wa wilaya na taasisi nyingine za serikali walipoteza kazi zao na kutupwa jela kwa makosa ya kuhusika na rushwa na ufisadi.
Korea Kaskazini
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ametangaza kwamba taifa hilo litafanyia majaribio silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu karibuni.
Amesema majaribio hayo yataimarisha uwezo wa taifa hilo kutekeleza mashambulio ya nyuklia, vyombo vya habari vya serikali nchini humo vimeripoti.
Kim Jong-un ametoa tangazo lake la karibuni zaidi alipokuwa akiongoza maonesho mwigo ya teknolojia ambayo inahitajika kuwezesha kombora lenye kilipuzi cha nyuklia kuingia tena ardhini baada ya kurushwa anga za juu, shirika la habari la KCNA limeripoti.
Shirika hilo limemnukuu akisema majaribio hayo yatafanyika “karibuni” lakini hakusema ni lini.
Korea Kaskazini imekuwa ikitoa msururu wa vitisho baada ya kuwekewa vikwazo vipya na Umoja wa Mataifa.
Lakini ingawa inajulikana kuwa ina silaha za nyuklia, wengi wanashuku uwezo wake wa kuzitumia.
Wiki iliyopita, Bw Kim alidai wanasayansi wa taifa hilo walikuwa wamefanikiwa kuunda kilipuzi cha nyuklia kidogo sana ambacho kinaweza kuwekwa kwenye makombora ya masafa marefu.
Mashirika ya habari ya serikali yalitoa picha ambazo zilidai kuonesha kilipuzi hicho.
Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema inatilia shaka madai ya Kaskazini na kusema haiamini taifa hilo limeweza kugundua teknolojia ya kuwezesha vilipuzi kuingia tena ardhini kutoka anga ya juu.
Mnamo Jumanne, Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye alionya kuwa iwapo Korea Kaskazini itaendelea na “uchokozi” na iwapo haitabadilisha msimamo wake basi inafuata njia ya kujiangamiza.
Mwezi Januari, Korea Kaskazini ilifanya jaribio lake la nne la nyuklia, na kusema lilikuwa bomu lenye nguvu sana la haidrojeni.
Hilo lilifuatiwa na kuzinduliwa kwa setilaiti kwa kutumia teknolojia ya makombora ambayo imepigwa marufuku.
Matukio yote mawili yalikiuka vikwazo vilivyowekwa vya Umoja wa Mataifa.
Katika wiki moja iliyopita, vikosi vya Marekani na Korea Kusini vimekuwa vikifanya mazoezi ya pamoja ambayo ndiyo makubwa zaidi kufanywa na nchi hizo mbili.












ge1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shehena ya sukari wakati alipotembelea ghala la kwanda cha Sukari cha Kagera akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ge2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shehena ya sukari wakati alipotembelea ghala la kwanda cha Sukari cha Kagera akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ge4
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shehena ya sukari wakati alipotembelea ghala la kwanda cha Sukari cha Kagera akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ge5
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mpaka kati ya Tanzania na Uganda kwenye Ranchi ya Missenyi mkoani Kagera Machi 14, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi,Festo Kiswaga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ge6
  Baadhi ya wananchi wa  Uganda waishio mpakani wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipotembelea kijiji cha Benkoma  wilayani Missenyi akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016. Wananchi hao wa Uganda walivuka mpaka ili kumuona  Waziri Mkuu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ge7
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Uganda waishio kwenye mpakani waliovuka mpaka ili kumuona wakati alipotembelea kijiji cha Benkoma wialyani Missenyi akiwa katika  ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ge8
Baadhi ya wananchi wa  Uganda waishio mpakani wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipotembelea kijiji cha Benkoma  wilayani Missenyi akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016. Wananchi hao wa Uganda walivuka mpaka ili kumuona  Waziri Mkuu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)