WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014, KIDATO CHA NNE MWAKA 2014
NA JKT MWAKA 2015 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI
UTANGULIZI:
Jeshi la polisi Tanzania linawajulisha kwamba litaendesha mafunzo ya awali ya Jeshi la
Polisi kwa miezi tisa katika shule ya Polisi Tanzania “Moshi” kuanzia taerehe
29/08/2015. Mafunzo hayo yatahusisha wahitimu wa vyuo vikuu, kidato cha sita kidato
cha nne wote wa mwaka 2014. Aidha wahitimu wa Jeshi la kujenga Taifa wa mwaka
2015 watahusika pia.
Maelekezo Muhimu.
1. Waliochaguliwa watatakiwa kuripoti kwa makamanda wa Polisi wa Mikoa Tarehe
28/08/2015 kwa ajili ya maandalizi ya usafiri wa kwenda shule ya Polisi Tanzania
tarehe 29/08/2015 kila mmoja atatakiwa kuwa na nauli ya kumwezesha kusafiri
toka makao makuu ya mkoa anakoanzia kusafiri hadi shule ya Polisi Moshi na
atarejeshewa nauli atakapofika chuoni baada ya kuwasilisha Tiketi ya safari.
2. Tarehe ya mwisho ya kuripoti chuoni ni tarehe 5/09/2015 na atakayeripoti baada ya
hapo hatapokelewa
3. Vijana hawa watalazimika kufika shuleni wakiwa na vitu vifuatavyo :
a) Vyeti vyao vyote vya masomo( original Academic Certificates/Result slip pamoja
na Leaving certificates) kidato cha Nne, Sita na vyuo. Vyeti halisi vya kuzaliwa
(Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
b) Mashuka mawili rangi ya Bluu bahari (light blue)
c) Chandarua chenye upana futi tatu
d) Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue naRaba)
e) Pasi ya Mkaa.
f) Ndoo moja.
g) Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu
(50,400/=).
h) Pesa kidogo ya kujikimu.
4. Kwa mujibu wa kanuni za shule ya Polisi ni marufuku kufika shuleni na simu ya
mkononi. Atakayepatikana na simu atafukuzwa shuleni hapo. Shule itaelekeza na
kusaidia kufanya mawasiliano.
5. Orodha ni kama ilivyo hapa hini:- KUANGALIA MAJINA YOTE BONYEZA HAPA
0 comments:
Post a Comment