
Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza ametimiza miaka 63 katika enzi.
Huo ni muda mrefu zaidi katika historia ya Uingereza.Alitawazwa kuwa malkia akiwa na umri wa miaka 25 pekee.

Mara ya kwanza alipofahamishwa kuwa ndiye atakayekuwa malkia wa Uingereza alikuwa nchini Kenya .

Alikuwa katika ziara rasmi nchini Kenya akiwa na mmewe Philip wakati huo akiwa na umri wa miaka 25 pekee.

Walikuwa wakikaa katika hoteli ya Treetops na jioni moja ikatangazwa kuwa babake amefariki akiwa usingizini.

Na hapo akawa Malkia lakini hakuambiwa habari hizo hadi alasiri siku iliyofuata.

Mmewe alimpeleka katika ikulu ndogo ya Sagana na kumpa habari kwamba sasa ndiye malkia wa Uingereza.

Sasa miaka 63 baadaye Malkia anawashukuru sana wote waliomtumia ujumbe wa heri njema.


Akizungumza karibu na mpaka wa Scotland Malkia Elizabeth 89 alisema ni heshima kubwa kwake kuendelea kuwahudumia waingereza.

Malkia Elizabeth amehudumu kwa siku 23,226 , yaani miaka 63 .


0 comments:
Post a Comment