Sunday, 6 September 2015

Beki wa Nigeria, William Ekong akibinuka tik tak dhidi ya mshambuliaji wa Tanzania, John Bocco katika mchezo wa leo
TANZANIA imejiweka njia panda katika mbio za Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017, baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Nigeria, jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Taifa Stars sasa inakamilisha mechi mbili za Kundi G bila ushindi, baada ya awali kufungwa mabao 3-0 na Misri mjini Alexandria Juni mwaka huu, wakati Nigeria inafikisha pointi nne baada ya awali kushinda 2-0 dhidi ya Chad.Kocha Charles Boniface Mkwasa aliwaanzisha wote washambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, lakini hii leo waliishia kuisumbua tu ngome ya Eagles.

Categories:

0 comments:

Post a Comment