Friday, 4 September 2015



Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, leo Septemba 4, 2015.
Baadhi ya wananchi wa Mji wa Kigoma Kusini, wakionyesha furaha yako kwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, leo Septemba 4, 2015.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akikaribishwa na Mwenyeji wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Kusini katika mwamvuli wa Ukawa kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, leo Septemba 4, 2015.Katikati ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe. 



01
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi ya CCM Bwana Abdallah Majura Bulembo wakiikingia katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam ambapo alifungua mkutano wa Makatibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM,Mkoa na Wilaya.03
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM ngazi ya,Mkoa na Wilaya uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.,06
Wajumbe wakishangilia wakati wa  ufunguzi wa Mkutano wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM ngazi ya,Mkoa na Wilaya uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam
Image copyrightEPA
Image captionWahamiaji waliookolewa katika pwani ya Libya
Zaidi ya watu hamsini hawajulikani waliko baada ya meli walimokuwa wakisafiria kuanza kuzama katika pwani ya Libya.
Msemaji wa shirika la kimataifa ya uhamiaji ameiambia BBC, kuwa wahamiaji wengine waliokuwa kwenye meli hiyo waliokolewa na wanajeshi wa majini wa Italia na wamepelekwa kisiwa cha Lampedusa.
Mwili wa mhamiaji mmoja pia uliopolewa baharini na kupelekwa katika kisiwa hicho.
Image copyrightEPA
Image captionMazishi wa Allan Kurdi, nduguye na mamake mjini Kobane
Miili ya mvulana mmoja kutoka Syria, Allan Kurdi na watu wengine kutoka familia yake imezikwa mjini Kobane nchini Syria, baada ya kusafirishwa kutoka Uturuki.
Babake Allan alivuka mpaka na kuingia eno linalothibitiwa na Wakurdi la Kobana akiwa na jeneza tatu.
Allan mwenye umri wa miaka mitatu na nduguye Galip mwenye umri wa miaka mitano na mama yao Rehan walifariki wakijaribu kuvuka mpaka na kuingia kisiwa cha Kos nchini Ugiriki.
Picha wa mwili wa mtoto huyo, katika ufuo wa bahari nchini Ugiriki, ilizua hamasa kote duniani, kuhusiana na hatma ya watu wanao kimbia vita vinavyoendelea nchini Syria.
Msafara wa magari yaliyokuwa yamebeba miili hiyo ilivuka mpaka na kuingia Kobane kutoka mji wa Suruc mpakani mwa Ugiriki
Babake Allan, Abdullah amesema familia yake waliangamia baada ya boti walimokuwa wakisafiria kuzama muda mfupi baada ya kutoka Uturuki.
Picha za mwili wa Allan, uliopatikana na ufuo wa bahari karibu na Bodrum, ilitoa hamasi kwa jamii ya kimataifa kutilia maanani wale wanaokimbia mapigano nchini Syria.
Aidha jamii ya Kimataifa imeshutumiwa kwa kutoshughulikia janga hilo ipasavyo.


Maelfu ya wahamiaji wameangamia baharini mwaka huu, wakijaribu kuingia Ulaya kupitia bahari ya Mediterenian.
Askofu Msaidizi wa jimbo katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini ameonesha kusikitishwa na kauli iliyotolewa hivi karibuni na Aliyekuwa katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa kuwa baadhi ya maaskofu wa kanisa hilo wamekuwa wakiohongwa fedha na wanasiasa akiwemo mgombea nafasi ya Urais Edward Lowassa. Akiongea na waandishi wa habari leo mjini Bukoba amesema kuwa anaamini kuwa Dr slaa aliteleza kutoa kauli hiyo.
Mgomea Mwenza wa Uraus kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wake wa kampeni aliofanya leo katika Kata ya Buza, jimbo la jijini Dar es Salaam.
Wananchi wakimshangilia Mama samia kwenye mkutano huo
MASHEIKH sita wa Tanzania waliochukuliwa mateka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wameachiwa huru usiku wa kuamkia jana.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Liberata Mulamula, alisema Balozi wa Tanzania nchini DRC kwa sasa yupo njiani kuelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo, Goma kwa ajili ya kuwaona mateka hao.
Alisema taarifa za kutekwa watu hao zilitolewa mwanzoni mwa Agosti mwaka huu ambapo Serikali ilifanya juhudi ya kufuatilia na kufanya uchunguzi juu ya taarifa hizo.
Mulamula alisema inasemekena watu hao wa taasisi ya kuhubiri dini ya Kiislamu walitekwa na kikundi cha waasi ambapo hadi sasa hakijajulikana.
Alisema watekaji wao walidai wapewe kiasi cha dola za Marekani 40,000 (sawa na Sh milioni 128.7 ) ili wawaachie Watanzania hao huru ambapo waliwaomba kupunguziwa hadi kufikia dola 20,000.
“Nchi yetu haijawahi kutokea kukamatwa mateka, lakini tunaipongeza Serikali ya DRC kulifuatilia hili na kutupatia taarifa,” alisema Mulamula.
Aliwataka wananchi wanaokwenda nchi za ugenini kutoa taarifa katika ubalozi au Wizara ya Mambo ya Ndani ili waweze kutambua haraka linapotokea tatizo kama hilo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya nje Zanzibar, Silima Kombo Haji, alisema watekaji hao walitumia ujanja wa kupiga simu kwa ndugu zao pamoja na watu wa karibu na Kijiji cha Goma.
Alisema juzi watekaji hao walikuwa wakipiga simu wakisisitiza kuwa muda umekwisha, hivyo fedha hizo zipelekwe haraka kabla hawajawadhuru.
Image copyrightGetty
Image captionKim Davies aliyekataa kusaini cheti cha ndoa Kentucky
Jaji mmoja nchini Marekani, ameagiza afisa mmoja wa serikali katika jimbo la Kentucky, kufungwa jela, baada ya kukataa kutekeleza agizo la mahakama la kutoa cheti rasmi cha ndoa, kwa wapenzi wawili wa jinsia moja.
Kim Davies amesema imani yake kama Mkristo, haimruhusu kusaini cheti kama hicho. Ndoa ya jinsia moja ilihalalishwa nchini Marekani Juni mwaka huu.
Umauzi huo wa Davis, wa kutosaini cheti hicho umepokelewa kwa hisia tofauti.
Kuna baadhi ya wale wanaomuona kama shujaa huku wengine wakisema ni msaliti.

Tofauti za imani

Davis ambaye ni karani wa mahakama, alikataa kutoa cheti hicho, kwa wanandoa hao katika kaunti ya Rowan iliyoko Kentucky.
Afisa huyo ambaye alichaguliwa na raia amesama, kitendo hicho kinakiuka maadili ya kidini.
Davis sasa ametupwa jela na jaji huyo kwa kudharau mahakama.
Amesema alikuwa amekula kiapo cha kuwa offisini na viapo vina maana nyingi.
Image captionWatu wanaoshabikia ndoa ya jinsia moja nje ya mahakama
Watu wanaoshabikia ndoa ya jinsia moja, walikusanyika nje ya mahakama, wakiimba kuwa mapenzi imeshinda na kusema kuwa sasa wanafuraha kwa sababu wanaweza kufunga ndoa.
Lakini kwa upande wake Kim Davis amepata uungwaji mkono kutoka kwa Wakristo wahafidina na baadhi ya wagombea wa urais wa chama cha Republican, ambao wanasema kuwa Davis amehukumiwa jela kwa kufuata imani zake

Thursday, 3 September 2015

5Wachezaji watatu wa kimataifa wa Tanzania wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi, Mrisho Ngasa (Free State – Afrika Kusini) Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta (TP Mazembe – Congo DRC) wamejiunga na kambi ya Taifa Stars iliyopo katika hoteli ya Urban Rose – Kisutu jana jijini Dar es salaam.Kocha Mkuu wa Taifa Stars Charels Mkwasa amewapokea wachezaji hao na jana kufanya mazoezi pamoja na wachezaji waliokuwa kambini nchini Uturuki saa 10 jioni katika uwanja Taifa jijini Dar salaam.Kwa mujibu wa ratiba ya kocha Mkwasa Stars leo alhamis itaendelea na mazoezi jioni saa 10 katika uwanja wa Taifa kabla ya kufanya mazoezi mepesi ya mwisho kesho ijumaa asubuhi.












 














Video ya Wildest DreamsImage copyrightUniversal
Image captionVideo ya Wildest Dreams iliyoandaliwa Botswana na Afrika Kusini
Mwelekezi wa video mpya ya Taylor Swift iliyoshutumiwa kwa kuonyesha picha mbaya ya Afrika amejitokeza na kuitetea vikali.
Video hiyo ya wimbo Wildest Dreams imedaiwa kuendeleza dhana potovu ya maisha bora iliyokuwa na wakoloni barani Afrika.
Lakini mwelekezi Joseph Kahn amesema "video hiyo haihusu ukoloni bali ni simulizi ya kisa cha mapenzi katika kundi la waandalizi filamu Afrika, 1950".
Swift hajazungumzia utata uliogubika video hiyo.
Kupitia taarifa, Kahn amekanusha madai kwamba video hiyo imeshirikisha Wazungu pekee.
“Ukweli ni kwamba sio tu kuwa kuna watu wa asili nyingine kwenye video hiyo, bali pia wabunifu waliofanyia kazi video hiyo ni wa asili nyingine.”
Ameeleza kuwa yeye ni wa asili ya Asia na Amerika, naye produsa wa video hiyo Jill Hardin na mhariri Chancler Haynes ni Waafrika Waamerika.
“Tuliamua kwa pamoja kwamba haingekuwa sahihi kihistoria kujaza waigizaji weusi kwenye video hiyo kwani tungeshutumiwa na kudaiwa kujaribu kuandika upya historia.
“Video hii inaonyesha mambo ya zamani kupitia watu wanaoishi kwa sasa na tunajivunia kazi yetu.”
"Kuna Waafrika weusi kwenye video hiyo, lakini sikuangazia sana watu wengine kwani muda mwingi unachukuliwa na Taylor na Scott (Eastwood).''
Video hiyo imetazamwa mara milioni 19 tangu ipakiwe mtandaoni Jumatatu
Image captionMilili ya wanajeshi wa Uganda waliouawa Somalia
Miili ya wanajeshi 10 wa Uganda, waliouawa na wapiganaji wa al-Shabaab, nchini Somalia imesafirishwa nyumbani.
Msemaji wa jeshi, Kanali Paddy Ankunda, amesema shambulio hilo "limebadili mambo" na al-Shabaab wanafaa kutarajia "jibu lifaalo".
Wanajeshi 12 wa Uganda waliuawa kwenye shambulio hilo la Jumanne, kwenye kambi ya wanajeshi wa Muungano wa Afrika (AU) Kusini mwa Somalia.
Al-Shabaab walisema waliua wanajeshi 70 wa AU.
Wanajeshi wa Uganda wamo kwenye kikosi cha wanajeshi 22,000 cha AU, kinachokabiliana na wapiganaji hao nchini Somalia.
Image captionMilili ya wanajeshi wa Uganda waliouawa Somalia
Kwenye tamko la kwanza kabisa kutoka kwa jeshi la Uganda kuhusu shambulio hilo, Kanali Ankunda alisema kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter: "Hatutalegeza juhudi zetu za kusaidia kurejesha amani Somalia licha ya shambulio hilo." Hakutoa maelezo kuhusu miili ya wanajeshi hao wengine wawili waliouawa.
Ripoti nyingine zinakadiria wanajeshi waliouawa kwenye uvamizi huo katika kambi ya Janale, kilomita 90 Kusini Magharibi mwa mji mkuu Mogadishu, ni kati ya 20 na 50.
Wakazi wanasema shambulio hilo lilianza kwa shambulio la kujitoa mhanga lililotekelezwa kwa kulipua gari lililotegwa bomu kwenye lango la kambi hiyo, na kisha kukawa na ufyatulianaji wa risasi uliodumu zaidi ya saa moja.
Image captionMilili ya wanajeshi wa Uganda waliouawa Somalia ikiwasili
Licha ya kupoteza ngome nyingi kusini na kati mwa Somalia, al-Shabaab wameendelea kushambulia vikosi vya serikali na Muungano wa Afrika pande mbalimbali nchini humo.
Wapiganaji hao pia hutekeleza mashambulio ya mara kwa mara ya kujitoa mhanga Mogadishu.
Image captionMilili ya wanajeshi wa Uganda waliouawa Somalia wakati ilipowasili Uganda