Sunday, 22 November 2015

Serikali ya Kenya imethibitisha kukamilika kwa maandalizi ya kumpokea kiongozi wa kanisa katoliki papa Francis.
Imebaki siku tatu tu kwa kiongozi huyo wa kanisa kuwasili nchini Kenya, huku viongozi wa kanisa la katoliki nchini humo pia wakithibitisha hilo.
Hii ni ziara ya kwanza ya Papa Francis barani Afrika, ambapo mbali na Kenya, pia ataitembelea Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Ubelgiji imewakamata watu 16 katika operesheni ya polisi kupambana na ugaidi mjini Brussels.
Katika msako huo, nyumba kumi na tisa zimekaguliwa, ingawa hakuna silaha au mabomu yaliyokamatwa.
Ingawa mtuhumiwa mkuu wa shambulio lililotokea mjini Paris, Salah Abdeslam, hajakamatwa.
Operesheni hiyo ya polisi kuhusiana na tishio la ugaidi mjini Brussels imemalizika bila kupatikana kwa vidhibitisho vya kutosha.
Hata hivyo mamlaka ya mji huo imeweza kuongeza muda ili kufanya uchunguzi Zaidi wa tukio hilo katika mji wa Brussels.
Kwa upande wake,Waziri Mkuu wa Ubelgiji , Charles Michel , amesema shule, vyuo vikuu vitafungwa , na usafiri wa treni ya ardhini utasitishwa.