![](http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/09/23/150923144026_kagame_paul_624x415_ap_nocredit.jpg)
Bunge la Senate la Rwanda limeidhinisha marekebisho katika katiba yatakayomuwezesha rais Paul Kagame kugombea urais kwa muhula wa tatu.
Bunge la ngazi ya chini lilipitisha azimio hilo mwezi uliopita lakini ni lazima lipigiwe kura ya maoni kabla ya kuidhinishwa kikamilifu.
Wafadhili wa kimataifa wameelezea wasiwasi kuhusu hatua ya Rais Kagame kugombea urais kwa muhula wa tatu baada ya kumaliza muhula wa sasa mwaka 2017.
Rais Kagame amesifiwa kwa kujenga upya nchi hiyo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 lakini wapinzani wanasema amekuwa akiwakandamiza wakosoaji wake
0 comments:
Post a Comment