Tuesday, 17 November 2015

Manusura wa mgodi nchini Tanzania walikula mende,vyura na hata wadudu wengine ili kuweza kuishi.
Kulingana na chombo cha habari cha AFP kilichomnukuu manusura mmoja kati ya watano waliokwama chini ya mgodi kwa siku 41,pia walikunywa maji machafu yaliokuwa yakitoka juu.
Chacha Wambura ambaye alikuwa akiongea na runinga ya taifa alinukuliwa akiongezea kuwa betri za tochi walizokuwa nazo zilizima na kulazimika kuwa ndani ya pango ambalo walilitumia awali kama eneo la kuwekea vifaa vyao.
Wachimba mgodi wengine 12 bado hawajulikani waliko kulingana na maafisa wa polisi.
Watano hao ni miongoni wachimba mgodi sita ambao walikuwa wakijaribu kuwaokoa wenzao 11 wakati mgodi huo ulipowaangukia.
Ijapokuwa waokoaji walikuwa wametumwa kuwatafuta sita hao,harakati hizo zilifutiliwa mbali baada ya juma moja huku waokoaji hao wakisema kuwa matumaini ya kuwapata wakiwa wazima yalididimia
Lakini juma hili baada ya wachimba migodi kusikia sauti usakaji wao ulianza mara moja.Wachimba migodi 11 waliokuwa wametoweka bado hawajapatikana na huenda wamefariki.

Categories:

0 comments:

Post a Comment