Thursday, 19 November 2015

Ligi kuu ya Hispania nayo itaendelea siku ya jumamosi baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa huku mchezo mkubwa ukiwa ni wa mahasimu Real Madrid na Barcelona.
Mchezo huu wa wapinzani hawa uliobatizwa jina la El Clasico utachezwa katika dimba la Santiago Bernabeu huku mashabiki wapatao 80,000 wakitazama mchezo huo katika uwanja huo.
Huku kukiwa na ahadi ya ulinzi wa kutosha kutoka kwa Polisi na wanausalama, hii inakuaja baada ya kutokea mashambulizi ya kigaidi nchini Ufaransa wiki hii.
Mvuto mkubwa wa mchezo huu ni kuwepo kwa nyota Cristiano Ronaldo wa real Madrid huku Leonel Messi wa Barca akiwa na hatihati baada baada ya kutoka kwenye majeruhi ya goti.
Mbali na mhezo wa El Clasico kutaigwa micheo mingine ya ligi hii
Real Sociedad na Sevilla
Espanyol na Malaga
Valencia na Las Palmas
Categories:

0 comments:

Post a Comment