Monday, 16 November 2015

Mtuhumiwa wa Ugaidi Ufaransa.
Jeshi la Polisi nchini Ufaransa  limetoa picha ya raia wa Ufaransa anayetafutwa akihusishwa na mashambulio ya jijini Paris yaliyoua watu 129.
Mtuhumiwa  huyo analikana kwa jina la Salah Abdeslam, mwenye miaka 26, anaelezwa kuwa mtu hatari.
Ripoti zinasema ametambuliwa kuwa alikodi gari lililotumika kwenye shambulio wakati yeye na watu wengine wawili waliposimamishwa na polisi karibu na mpaka wa Ubelgiji.
Imeelezwa kuwa maafisa walimruhusu kuendelea na safari yake baada ya kutazama kitambulisho chake.
Categories:

0 comments:

Post a Comment