Thursday, 19 November 2015

Mbunge wa Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa ameidhinishwa na Bunge la Tanzania kuwa waziri mkuu mpya wa taifa hilo.
Bw Majaliwa amepata kura 258 kati ya 351 zilizopigwa, baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kutangazia bunge kwamba ndiye aliyekuwa amependekezwa na Rais John Pombe Magufuli awe Waziri Mkuu.
Bw Majaliwa, 55, amekuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa, Jimbo la Lindi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) tangu 2010.
Eneo la Ruangwa linapatikana kusini mashariki mwa Tanzania.
Alikuwa naibu waziri katika afisi ya Waziri Mkuu aliyehusika na utawala wa mikoa na serikali za mitaa katika serikali ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete.
Anatarajiwa kuapishwa kesho katika ikulu ya Dodoma.
Bw Majaliwa, ambaye ni mwalimu kitaaluma, atamrithi Mizengo Pinda ambaye alihudumu kama Waziri Mkuu chini ya Rais mstaafu Kikwete kuanzia 2008.
Categories:

0 comments:

Post a Comment