Tuesday, 17 November 2015

Afrika Kusini imetia saini makubaliano na Marekani kuruhusu Marekani kuuza kuku wake nchini humo.
Makubaliano hayo yanatarajiwa kuondoa wasiwasi kati ya mataifa hayo baada ya Marekani kutishia kusimamisha manufaa ya biashara za bidhaa za kilimo inayopata Afrika Kusini kufuata mgogoro huo wa kuku.
Afrika Kusini ina wasiwasi kwamba mlipuko wa ugonjwa wa homa ya kuku ambao umewaua takriban ndege milioni 50 huenda ikasababisha hatari ya kiafya miongoni mwa wanyama na binaadamu.
Kuku ni chakula kinachopendwa sana Afrika kusini na wakosoaji wana wasiwasi kwamba Marekani itapeleka kuku wa ziada katika taifa hilo,hatua ambayo wanasema itaathiri pakubwa bishara ya nyama hiyo nchini humo.
Categories:

0 comments:

Post a Comment