Watu wanne akiwemo mtoto wa miezi
sita na polisi mmoja, wameuawa kwa kupigwa risasi kwenye kambi moja ya
wahamiaji nchini Ufaransa.
Polisi wanasema mwanaume mmoja akiwa na
bunduki ya uwindaji alimfyatulia risasi mtoto, mwanamume na mwanamke
baada ya kutokuelewana jambo kaskazini mwa nchi hiyo, na kisha
kumfyatulia risasi polisi mmoja aliyeingilia kati na kumuua ofisa mmoja.Mtoto wa miaka mitatu, ambaye yupo mahututi hospitalini, pamoja na mtu mwingine mmoja pia walijeruhiwa kabla ya polisi kumfyatulia risasi mtu huyo miguuni.
Taarifa zinasema kuwa mtu huyo anatokea katika jamii moja ya wahamiaji.
Vurugu zilitokea katika kambi hiyo huku wahamiaji wenye hasira wakijaribu kumvamia mwandishi wa habari aliyekua anachukua tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment