Wednesday, 26 August 2015


Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan, akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni aliofanya katika mji mdogo wa Tarakea, jimbo la Rombo, mkoani Kilimanjaro

Mgombea mwenza wa Urais kupitia chama cha mapinduzi, CCM SAMIA SULUHU HASSAN amewahakikishia wakazi wa TARAKEA wilayani ROMBO mkoani KILIMANJARO kuwa ujenzi wa shule ya KENI utamalizika baada ya kusimama kwa muda.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara ambao ni mwendelezo wa kampeni za CCM SAMIA amesema iwapo CCM itapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi itahakikisha shule hiyo inakamilika ili ichukue  idadi kubwa ya wanafunzi kwa kuongeza madarasa na mabweni.
Mgombea mwenza wa Urais pia amefanya mkutano wa hadhara katika eneo la MARANGU mtoni wilayani MOSHI na kuahidi kuwapatia vijana wa eneo hilo pikipiki thelathini ili kujikwamua kimaisha

0 comments:

Post a Comment