Wednesday, 26 August 2015

VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Jimbo la Morogoro Mjini vimezindua kampeni zao kwa kumnadi mgombea wa ubunge kupitia Chadema, Marcossy Albanie pamoja na wagombea wa udiwani kwa kata 29.
Walizindua kampeni juzi mjini hapa.
Mgombea huyo wa ubunge alitaja vipaumbele atakavyo vishughukikia ndani ya miezi sita akichaguliwa, ni pamoja na kuondoa kero ya maji, afya elimu, ajira kwa vijana na kufufua viwanda vilivyopo Manispaa ya Morogoro.
Alitaja eneo jingine ni kusimamia rasilimali za nchi zinufaishe watu wote hususani katika Manispaa ya Morogoro. Katibu wa Chadema, Wilaya ya Morogoro Mjini kichama, Esther Tawete, alisema Chadema imeanza safari katika kusimamia masuala ya uchumi, siasa na utawala bora.
Categories:

0 comments:

Post a Comment