Polisi nchini Marekani imesema muuaji wa Waandishi wawili wa habari nchini Marekani amefariki.
Ujumbe
unaoonekana kutumwa na mtu aliyekuwa na silaha nchini Marekani na
kuwaua kwa risasi watangazaji hao wawili wa televisheni wakati wa
matangazo ya moja kwa moja unaashiria kwamba alikuwa na uchungu kwa
kinachoonekana kuwa ubaguzi wa rangi.Vester Lee Flanagan, aliyefutwa kazi katika kituo hicho cha televisheni alifariki baada ya kujipiga risasi, saa chache baadaye.
Msimaizi wa kituo hicho cha televisheni alimtaja mshambuliaji huyo kuwa mtu asiyekuwa na furaha ambaye ilikuwa vigumu kufanya naye kazi.
0 comments:
Post a Comment