Wednesday, 26 August 2015


Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi katika mkutano wa Mwaka wa Wadau wa Barabara wa TAMISEMI uliofanyika katika hoteli ya Ngurdoto wilayni Arumeru Mkoani Arusha 
 
Rais JAKAYA KIKWETE ameitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI na wadau wa barabara kuongeza juhudi katika utengenezaji wa barabara vijini ili ziweze kupitika wakati wa kiangazi na masika.

Rais KIKWETE ameyasema hayo Mkoani ARUSHA wakati akifungua Mkutano wa NNE wa Wadau wa Barabara nchini ambapo amesema bila kuunganisha barabara za vijijini na mikoa mikubwa hakuna mafanikio ya haraka na itakuwa ni kazi bure.
       
Amesema Serikali imeanzisha Idara ya Miundombinu itakayokuwa na Vitengo VITATU vya Utafiti wa Barabara za Mijini na Vijijini ili kurahisisha kwa ukaribu ujenzi wa barabara nchini.
Rais KIKWET amesema Kitengo cha Utafiti kitasaidia Mfuko wa Barabara kuweza kujua kiwango cha fedha za matengenezo kinachohitajika baada ya kufanyika utafiti.

Aidha amewataka wadau hao kuhakikisha wanapitisha wakandarasi wenye sifa ili waweze kujenga barabara zenye viwango na kuacha rushwa ambazo amesema zinarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

0 comments:

Post a Comment