Tuesday, 12 January 2016

Rais wa marekani Barack Obama ameamrisha kuwa mazao ya kilimo kutoka Afrika Kusini yaanze kutoswa ushuru ifikapo kati kati ya mwezi Machi ikiwa serikali ya Afrika kusini itashindwa kutekeleza makubaliano ya kibiashara yaliyoafikiwa wiki iliyopita.
Baada ya miezi kadha ya mazungumzo kuhusu ubora wa bidhaaa za kuku na nguruwe kutoka nchini Marekani, makubaliano yaliafikiwa ambayo yataruhusu bidhha kutoka Afrika Kusini kuuzwa nchini Marekani bila kutoswa ushuru nchini ya makualino ya (Agoa)
Mzozo wa kibiashara kati ya marekani na Afrika Kusini ulitokana na suala kuwa bidhaa za kuku kutoka Marekani, kuwa havikuwa na ubora lakini iliafikiwa kuwa tani 65,000 za kuku zitauzwa nchini Afrika Kusini.
Tarehe ya mwisho ya mwezi Machi ni onyo kutoka kwa ikulu ya marekani kuwa ikiwa hilo haliwezi kutekelezwa, kutakuwa na athati ikiwemo kutosa ushuru kwa bidha kadha za kilimo za afrika kusini.
Categories:

0 comments:

Post a Comment