Wasichana waliotekwa na Boko Haram.
Mamia ya ndugu wa wasichana wa Chibok nchini Nigeria waliotekwa na kundi la wapiganaji la Boko Haram wamefanya mkutano ndani na Rais wa taifa hilo Muhammadu Buhari wakishinikiza kuendelea kuwatafuta wasichana Zaidi ya 200 waliotoweka tangu 2014.
Wakiwa wamevalia fulana nyekundu zilizoandikwa ujumbe wa Bring back out girls,wanafamilia hao waliingia katika chumba maalumu kwaajili ya mkutano wa ndani na Rais. Pamoja na kwamba hadi sasa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu,watoto wao watekwe na Boko haram lakini bado wazazi hawa wanatafuta majibu ya maswali ya kwamba wapi walipo watoto wao. Wanandugu hao wamedai kuwa Rais Buhari aliwahakikishia kwamba atafanya kila linalowezekana kuhakikisha wasichana hao wanapatikana.
Lakini wamesema kuwa kwa sasa wanahasira na serikali na ambapo wamerusha lawama kuwa serikali haina kitengo imara cha upelezi ili kuweza kujua waliko wasichana. Mmoja wa Baba wa watoto waliotekwa,ameiambia BBC kuwa yeye hatapumnzika hadi siku atakapo muona mtoto wake.Kitendo cha kutekwa kwa wasichana wa Chibok kumesababisha mataifa mbali mbali ya afrika na duni kulaani.
0 comments:
Post a Comment