Wachezaji watatu wa kimataifa wa Tanzania wanacheza soka la kulipwa nje ya nchi, Mrisho Ngasa (Free State – Afrika Kusini) Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta (TP Mazembe – Congo DRC) wamejiunga na kambi ya Taifa Stars iliyopo katika hoteli ya Urban Rose – Kisutu jana jijini Dar es salaam.Kocha Mkuu wa Taifa Stars Charels Mkwasa amewapokea wachezaji hao na jana kufanya mazoezi pamoja na wachezaji waliokuwa kambini nchini Uturuki saa 10 jioni katika uwanja Taifa jijini Dar salaam.Kwa mujibu wa ratiba ya kocha Mkwasa Stars leo alhamis itaendelea na mazoezi jioni saa 10 katika uwanja wa Taifa kabla ya kufanya mazoezi mepesi ya mwisho kesho ijumaa asubuhi.
Thursday, 3 September 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment