![](http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/09/04/150904114903_syria_kobane_funeral_624x351_epa_nocredit.jpg)
Miili ya mvulana mmoja kutoka Syria, Allan Kurdi na watu wengine kutoka familia yake imezikwa mjini Kobane nchini Syria, baada ya kusafirishwa kutoka Uturuki.
Babake Allan alivuka mpaka na kuingia eno linalothibitiwa na Wakurdi la Kobana akiwa na jeneza tatu.
Allan mwenye umri wa miaka mitatu na nduguye Galip mwenye umri wa miaka mitano na mama yao Rehan walifariki wakijaribu kuvuka mpaka na kuingia kisiwa cha Kos nchini Ugiriki.
Picha wa mwili wa mtoto huyo, katika ufuo wa bahari nchini Ugiriki, ilizua hamasa kote duniani, kuhusiana na hatma ya watu wanao kimbia vita vinavyoendelea nchini Syria.
Msafara wa magari yaliyokuwa yamebeba miili hiyo ilivuka mpaka na kuingia Kobane kutoka mji wa Suruc mpakani mwa Ugiriki
![](http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/624/amz/worldservice/live/assets/images/2015/09/04/150904115703_mazishi_ya_allan_kurdi_512x288_bbc_nocredit.jpg)
Babake Allan, Abdullah amesema familia yake waliangamia baada ya boti walimokuwa wakisafiria kuzama muda mfupi baada ya kutoka Uturuki.
Picha za mwili wa Allan, uliopatikana na ufuo wa bahari karibu na Bodrum, ilitoa hamasi kwa jamii ya kimataifa kutilia maanani wale wanaokimbia mapigano nchini Syria.
Aidha jamii ya Kimataifa imeshutumiwa kwa kutoshughulikia janga hilo ipasavyo.
Maelfu ya wahamiaji wameangamia baharini mwaka huu, wakijaribu kuingia Ulaya kupitia bahari ya Mediterenian.
0 comments:
Post a Comment