![Mtawa](http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2016/03/09/160309100809_women_favourite1_624x351_afp_nocredit.jpg)
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ametangaza kwamba Mother Teresa atafanywa mtakatifu Septemba mwaka huu.
Sherehe ya kumtawaza kuwa mtakatifu itafanyika tarehe 4 Septemba.Njia ya kumfanya mtakatifu ilifunguliwa Desemba mwaka jana baada ya Vatican kutambua muujiza wa pili uliohusishwa naye. Muujiza huo alipokea mwanamme raia wa Brazil ambaye alipona saratani kwenye ubongo wake.
Mother Teresa alipewa tuzo ya amani ya Nobel kutokana na huduma yake kwa raia maskini kwenye vitongoji wa jimbo la Kolkata nchini India.
Alifariki dunia mwaka 1997.
![Papa](http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/624/amz/worldservice/live/assets/images/2015/12/18/151218113524_mother_teresa__640x360_afp_nocredit.jpg)
0 comments:
Post a Comment