![](http://ichef-1.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/06/16/150616194009_bashir_sudan_640x360_reuters_nocredit.jpg)
Serikali ya Sudan Kusini imefeli
kubatilisha uamuzi wa mahakama unaoishtumu kwa kukataa kumkamata rais wa
Sudan Omal al- Bashir wakati alipohudhuria mkutano wa AU mnamno mwezi
juni.
Kushindwa kwa serikali kutekeleza agizo la kumkamata
lililotolewa na mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC ni
kinyume na sheria za taifa hilo,mahakama ya rufaa iliamuru.Mahakama ya chini ilitoa uamuzi kama huo,na serikali ina matumaini kwamba itashinda rufaa.
Inahoji kwamba Bashir ana haki ya kinga ya kirais.
0 comments:
Post a Comment