
Wengi wa wahamiaji hao walikuwa katika hali mbaya wengi wakiwa hawana maji mwilini,kulingana na kamanda wa polisi Peter Kakamba.
''Baada ya kuwakamata tulilazimika kuwatafutia wauguzi ili wawekwe maji mwilini,walikuwa na njaa,na wasiojiweza,walikuwa wamelaliana katika lori hilo,tuliwapatia huduma ya kwanza na kuwalisha uji kabla ya kuwaleta Iringa mjini''.
Tanzania na Malawi hutumiwa kama vituo muhimi vya watu wanaotoroka kiangazi na migogoro nchini Ethiopia na Somalia ili kuweza kufika Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment