Monday, 18 January 2016

Buyelakhaya Dalindyebo.
Mfalme wa aba Thembu nchini Afrika Kusini anayehudumia kifungo jela Buyelakhaya Dalindyebo amelazwa hospitalini mashariki mwa London akiugua ugonjwa usiojulikana,kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini Afrika Kusini.
Hii ni mara ya pili kwa yeye kulazwa hospitalini katika kipindi cha wiki za hivi karibuni baada ya mfalme huyo kupelekwa katika hospitali moja nchini humo alipofanya mgomo wa kula.
Ripoti hizo zilisema kwamba anaugua vidonda vya tumbo na shinikizo ya akili.
Kulingana na gazeti la the New Age,idara ya kurekebishia watu tabia imesema kuwa hali yake ilizorota mda mchache tu baada ya kutakiwa kuondoka hospitalini.
Mfalme Dalindyebo anatoka katika ukoo wa aba Thembu pamoja na aliyekuwa rais wa taifa hilo Marehemu Nelson Mandela.
Alianza kuhudumia kifungo chake cha miaka 12 jela kwa utekeji nyara,unyanyasaji na kuchoma nyumba moto baada ya harakati za kujaribu kufutilia mbali hukumu hiyo.
Kesi dhidi yake inahusiana na mgogoro wa miongo miwili aliokuwa nao na wafuasi wake.
Categories:

0 comments:

Post a Comment