

Ndege hiyo, iliyokuwa safarini kuelekea mji wa Paloch katika jimbo la Upper Nile ilianguka kwenye ukingo wa mashariki wa Mto Nile. Maafisa bado wanatafuta manusura. Msemaji wa rais wa Sudan Kusini Ateny Wek Ateny ameambia shirika la habari la Reuters kwamba mhudumu mmoja wa ndege hiyo pamoja na mtoto, ambao walikuwa kwenye ndege hiyo, wamenusurika.

Ubalozi wa Urusi nchini Uganda, ambao pia husimamia Sudan Kusini, umesema unawasiliana na maafisa wa serikali Juba kupata habari zaidi, kwa mujibu wa msemaji wake Radmir Gainanov.
Ajali hiyo imetokea siku chache tu baada ya ndege nyingine ya Urusi kuanguka eneo la Sinai, Misri Jumamosi.
Chanzo:BBC
0 comments:
Post a Comment